Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho. (Picha zote na Ramadhan Othman, Dodoma)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo, kuhudhuria katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kinachoanza jioni hii mjini humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM), alipowasili Uwanja wa Ndege wa Dodoma leo, akihudhuria katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa kinachoanza jioni hii. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.
Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu Dodoma, wakimlaki Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alipowasili kihudhuria kikao hicho mjini Dodoma leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (kulia), akiimba wimbo wa Chama alipokaribishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Makao Makuu Dodoma leo, mara liowasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi.
No comments:
Post a Comment