TANGAZO


Saturday, February 15, 2014

Balozi Seif atoa msaada wa Mabati Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina, awasili Dodoma kuhudhuria kikao cha NEC

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi Mchango wa Mabati 126 kati ya 236 aliyoahidi kuchangia kwa ajili ya uwezekaji wa Tawi Jipya la CCM Mombasa Kwamchina, linalojengwa kwa nguvu za wanachama wenyewe wa tawi hilo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akipungia mkono wana CCM na baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma tayari kushiriki kwenye kikao cha NEC pamoja na Bunge la Katiba, mjini Dodoma leo.
Baadhi ya vikundi vya uhamasishaji na Utamaduni vikitumbuiza  wakati Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma kuhudhuria Kikao cha NEC.
Balozi Seif Ali Iddi na mkewe, Mama Asha Suleiman Iddi wakiangalia moja ya vikundi vya uhamasishaji vilivyowapokea wakati wakiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Dodoma. (Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.)

Na Othman Khamis Ame, OMPR
Wakati Tanzania inakaribia kuingia kwenye uchaguzi Mkuu wa Tano mwakani unaoendelea kuhusisha mfumo wa vyama vingi vya Kisiasa tokea mwaka 1995 Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wametahadharishwa kujiepusha na tabia za vikundi miongoni mwao ambavyo vinaweza kupunguza nguvu za chama hicho katika dhana nzima ya  kuendelea kushika dola.
Tahadhari hiyo imetolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi wakati wa hafla fupi na kukabidhi mchango wa Mabati ya kuezekea  136 kati ya 236 yanayohitajika kutekeleza ahadi yake kwa
Uongozi wa Tawi la CCM Mombasa kwa Mchina Wilaya ya
Magharibi akiwa pia muanzilishi wa Tawi hilo.
Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema bado ana imani thabiti kwamba amani ya Taifa la Tanzania itaendelea kubakia ndani ya mikono ya Chama cha Mapinduzi kinachohubiri Umoja, Mshikamano na upendo miongoni mwa Wananachi wote.
“Tusiichezee shilingi chooni akimaanisha kutahadharisha wanachama hao pamoja na Wananchi kuilinda amani  ya nchi ambayo ndio muhimili wa jamii katika harakati za maendeleo “. Alisema Balozi Seif.
Alisema tabia ya makundi inayoonekana kujipenyeza ndani ya Chama hicho tokea uchaguzi wa mwaka 2010 ikiendelea kushikiwa bango na baadhi ya Viongozi inaweza kuijengea mazingira magumu CCM katika uchaguzi Mkuu ujao hapo Mwakani.

No comments:

Post a Comment