TANGAZO


Friday, January 24, 2014

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid atoa Tamko la Siku ya Ukoma Duniani


Waziri wa  Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.  Seif  Rashidi (kulia), akitoa tamko kuhusu Siku ya Ukoma Duniani na mtu ambaye hana vimelea hivyo. Kushoto ni  Katibu Mkuu wazara hiyo Charles  Pallangyo. (Picha  na Magreth Kinabo)
 
 
Na Magreth Kinabo
WAZIRI wa   Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.  Seif  Rashidi  ameitaka jamii kuwahi mapema katika vituo vya afya ili kuweza kupata uchunguzi pindi wanapoona mabaka ya aina yoyote katika ngozi ya mwili ili kuweza kupata tiba sahihi ya ugonjwa  wa ukoma  na kuepusha ulemavu usio wa lazima.
 Kauli hiyo imetolewa na Waziri huyo, alipokuwa akitoa tamko kuhusu Siku ya Ukoma Duniani itakayoadhimishwa  nchini  Kimkoa Januari 26, mwaka huu, katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo leo, jijini Dares Salaam.
Alisema Tanzania ni miongoni wa nchi 17 duniani ambazo zina viwango bado zina viwango vya juu wa ugonjwa wa ukoma.
“Athari  kuu ya ugonjwa wa ukoma ni ulemavu wa kudumu . Ulemavu unatokana na kuchelewa kwa uchunguzi na matibabu sahihi . Tujenge tabia ya kuchunguza miili yetu na pale  tunapoona mabadiliko yoyote yanajitokeza twende mapema katika vituo vyetu  vya huduma  kuchunguzwa ili tupate  ushauri na matibabau stahili,” alisema Dk.  Rashidi.
Dk. Rashidi  asilimia  11  ya wagonjwa wapya  wa ukoma  wanaojiotokeza  katika vituo vyetu kwa ajili ya uchunguzi na kuanza matibabu wanakuwa tayari wana ulemavu wa  kudumu .
  Aliongeza kuwa ugonjwa huo   hutibiwa na dawa mseto (Multi drug theray au MDT) na zipo za kutosha.
 Alisema takwimu za   hapa nchini kwa miaka mitano iliyopita zinaonesha kuwa idadi  ya wagonjwa wapya wa ukoma inazidi kupungua kutoka 3,248 mnamo mwaka 2008 hadi 2,548 kwa mwaka 2012 .
 Aliongeza  kuwa bado kuna wilaya 15 ambazo hazijafikia kiwango cha kutokomeza ugonjwa huo cha chini mgonjwa 1 kati ya watu 10,000 katika jamii husika. Alizitaja wilaya wilaya hizo  ni Liwale ,Nachingwea,Mkinga,Pangani, Muheza, Rwangwa, Mvomero, Kilwa, Msasi, Chato, Nanyumbu,Lindi Kisarawe,Newala na Songea.
Alizitaka halimashauri  ambazo zina wagonjwa wengi, kutenga fedha kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kutambua dalili za wali  za ukoma ili kuwahi matibabu na kuzuia maambukizi mapya .
Dk. Changamoto  wanazokabiliana  katika kupambana na ugonjwa huo, watumishi wa afya kutambua kwa urahisi ugonjwa huo, jamii kuendelea kushikilia imani potofu  na kuchelewa kujitokeza kupata matibabu hadi wanapopata ulemavu.
 Ugonjwa  huo ni wa kuambukia unaoletwa na vimelea hai  na unasambazwa kwa njia ya hewa kutoka kwa mgonjwa kwenda k wa mtu ambaye hana vimelea hivyo.

No comments:

Post a Comment