Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko, akiongea na Ujumbe kutoka Serikali ya China kuhusu Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina na maadhimisho ya Miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho. Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akisikiliza jambo kutoka kwa Mshauri wa Utamaduni kutoka Ubalozi wa China nchini Liu Dong wakati ujumbe huo ulipomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadili kuhusu maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina na maadhimisho ya miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko akisisitiza jambo kwa ujumbe wa Serikali ya China juu ya maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Kichina na maadhimisho ya miaka 50 ya Kidiplomasia baina ya China na Tanzania yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru kesho. Wa pili kulia ni Mratibu wa Ujumbe huo, Zhou Hong.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko (kulia), akipokea Kitabu chenye Historia ya Mchezo wa Karate kutoka kwa mmoja wa wachezaji wa Mchezo huo kutoka China, Shi yan Cen (kushoto), ikiwa ni ishara ya kuendelea kudumisha ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na China.(Picha zote na Benjamin Sawe wa Wizara ya Habari, Maelezo)
No comments:
Post a Comment