Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kuidhinisha mswada
ambao ikiwa utaidhinishwa utatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya
jinsia moja.
Museveni amemuandikia spika wa bunge barua na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha
mswada huo Disemba mwaka jana bila ya kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge.Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja ikiwemo kufungwa jela na pia ni uhalifu kwa mtu yeyote kukosa kuripoti visa vya mapenzi ya jinsia moja.
Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia unapendekeza kuadhibiwa kwa watu wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja bila ya kuwakashifu kwani wanaweza kufungwa jela.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais Museveni amesema kwamba mswada huo ulishinikizwa zaidi kupitishwa na wabunge licha ya kuwashauri kusubiri hadi serikali itakapoutathmini.
Rais anaelewa kwamba ikiwa atauidhinisha mswada huo na kuufanya sheria kutakua na ukosoaji mkubwa kutoka kote hali inatakayochangia baadhi ya nchi za kigeni kusitisha msaada kwa Uganda.
No comments:
Post a Comment