TANGAZO


Friday, January 17, 2014

Mtevu atoa madawati 500 kwa Shule za Msingi jimboni kwakeTemeke

 Madiwani wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (wa pili kushoto)  kukata utepe  wakati wa hafla ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika Shule za msingi katika Kata 13 za jimbo hilo. Hafla hiyo imefanyika leo Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
 Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu akizungumza baada ya kukabidhi madawati 500 yenye thamani ya sh. mil. 67.5 yatakayogawiwa katika shule zilizopo katika Kata 13 za Jimbo hilo. Madawati hayo yaliyonunuliwa kwa fedha za Mfuko wa Jimbo yalikabidhiwa kwa madiwani wa Kata hizo katika hafla iliyofanyika Chuo cha Ufundi Chang'ombe, Dar es Salaam.
 Naibu Meya wa wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga akitoa shukurani kwa Mbunge Mtemvu kutoa madawati hayo.
 Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Zena Mgaya akimpongeza Mtemvu kwa juhudi za kuinua kiwango cha elimu wilayani Temeke.
 Ofisa Elimu wa  Shule za Msingi Manispaa ya Temeke, Honorina Mumba akieleze furaha ya kupata madawati hao 500 yatakayopunguza tatizo la madawati wilayani Temeke.
Mtemvu akiangalia wakati mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi akiandika jina lake.
 mwanafunzi Azizi Ally wa Shule ya Msingi Keko Magurumbasi, akitoa shukurani kwa Mtemvu kwa  niaba ya wanafunzi kwa kuwapatia madawati hayo . 
Fundi akiendelea kupiga msasa baadhi ya madawati hayo yalitotengenezwa VETA Chang'ombe

No comments:

Post a Comment