TANGAZO


Monday, January 13, 2014

Buriani Ariel Sharon

 

Wageni waliofika kwa ibada maalum ya Sharon walimsifu kama kiongozi aliyepigania waisraeli
Ibaada maalum ya aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ariel Sharon imefanyika nje ya majengo ya bunge la Israel.
Bwana Sharon atakumbukwa kwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa taifa la Israel lakini pia alikuwa mwanajeshi na mwanasiasa jasiri aliyechukiwa na wapalestina wengi.
 
Waliohutubia umati,wamemtaja Sharon kama mtu aliyejitolea kuhakikisha kuna usalama kwa watu wake.
Waziri mkuu Benjamin Netanyahu alisema kuwa Sharon alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa wayahudi na ambaye atakumbukwa zaidi ya wote.
Licha ya sifa hizo Bwana Sharon anachukiwa sana na waarabu hasa wapalestina kwa dhuluma alizowatendea chini ya utawala wake.
Kiongozi huyo aliaga dunia siku ya Jumamaosi akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuwa hali mahututi kwa takriban miaka minane.
Atazikwa baadaye leo katika shamba la familia yake jangwani Negev.
Maelfu ya waombolezaji walitoa heshima zao za mwisho kwa Sharon siku ya Jumapili wakati ambapo mwili wake ulikuwa umelazwa nje ya majengo ya bunge mjini Jerusalem.

No comments:

Post a Comment