Mamia ya wanajeshi walioasi jeshi katika Jamhuri ya Afrika ya
Kati,wameanza tena kurejea kazini katika mji mkuu wa Bangui.
Wengi walioasi walikuwa Wakristo waliohofia kuwa huenda wakashambuliwa na
wenzao waisilamu baada ya mapinduzi ya mwaka uliopita yaliyoongozwa na Waislamu
wengi waasi wa kundi la Seleka.Taifa la Jamhuri ya Afrika ya Kati, limekumbwa na mapigano ya kidini kwa karibu mwaka mmoja sasa lakini Rais wa mpito wa sasa, Alexandre-Ferdinand Nguendet, ametangaza kuwa wakati wa ghasia umefika kikomo nchini humo.
Alisema kuwa amewaonya waasi na waporaji kuwa wakati wao wa kusherehekea vya bure umekamilika.
Hata hivyo BBC imepokea habari za kusikitisha ambapo mkaazi mmoja wa Bangui alionekana akila nyama ya Mwislamu aliyekuwa ameuliwa na umma.
No comments:
Post a Comment