TANGAZO


Monday, December 23, 2013

Ufungaji wa maadhimisho ya Wiki ya Chakula Salama, Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Raymond Wigenge akitoa maelezo kuhusiana na Wiki ya Chakula Salama, katika kilele cha ufungaji wa maonesho ya Wiki ya Chakula Salama jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando, akizungumza katika ufungaji wa maadhimisho ya Wiki ya Chakula Salaam, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa akihutubia wananchi (hawapo pichani), wakati akifunga maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Chakula Salama katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Elias Chinamo.

Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa (hayupo pichani), wakati akihutubia  alipokuwa akifunga maonesho ya Wiki wa Chakula Salama, Viwanja vya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uledi Mussa akihutubia wananchi (hawapo pichani), wakati akifunga maonesho ya maadhimisho ya Wiki ya Chakula Salama katika Viwanja vya Mnazi Mmoja mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Donan Mmbando na kulia ni Mkurugenzi wa Kinga  wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Elias Chinamo. (Picha zote na Gaudensia Simwanza wa TFDA)

No comments:

Post a Comment