|
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika maeneo yanayohusu Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji,wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Omar Issa.
|
|
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakitia saini mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakitia saini Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakibadilishana hati ya mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakibadilishana hati ya Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
|
|
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza akieleza malengo ya Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania ikiwa ni kuanzisha na kuendeleza ufugaji kisasa wa nyuki unaojali mazingira, unaozalisha bidhaa bora za ufugaji nyuki zitakazomwingizia mfugaji kipato cha kutosha na kumwezesha kuchangia kikamilifu pato la Taifa. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara.
|
|
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mipango iliyowekwa katika kuhakikisha sekta ya ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali inaendelea kukua, wakati wa hafla ya utiaji saini kwa ajili ya programu endelevu ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali katika kanda ya mashariki,kati na magharibi mwa Tanzania.kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza.
|
|
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi serikali ya awamu ya nne inavyoendelea kusaidia mpango wa ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali ili kuhahakikisha ukuaji katika sekta hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.kushoto ni katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
|
Na Hassan Silayo-MAELEZO
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuhamasisha na kuvutia miradi ya uwekezaji nchini kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati wa hafla ya utiani saini wa hati ya mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo.
Dkt. Nagu alisema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini kwa kuboresha na kutekeleza sera na sheria zitakazovutia uwekezaji kwani inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania.
“kutokana na jitihada za serikali za kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, idadi na thamani ya miradi iliyoidhinishwa na kituo cha uwekezaji Tanzania imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na hii inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania”Alisema Dkt.Nagu.
Dkt. Nagu aliongeza kuwa ili kuendelea kuboresha Sera na Sheria za uwekezaji ili ziendane na mazingira na mahitaji ya uwekezaji serikali imeshakamilisha maandalizi ya Taarifa ya Mapitia ya Sera zinazohusu uwekezaji yaliyofanyika kwa kutumia mfumo wa kutathmini Sera za Uwekezaji unaotumiwa na shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo(OECD).
Katika ushiriki wa Serikali katika utoaji elimu ya ujasiriamali Dkt. Nagu alisema kuwa serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ujasiriamali nchini hasa wale wa vijijini.
Serikali imetekeleza Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira ambapo tathmini iliyofanyika inaonesha mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 50.03 imetolewa kwa utaratibu wa serikali kutoa Dhamana ya mikopo kwenye benki za CRD NA NMB, mpango ulionufaisha wajasiriamali 74,701.
No comments:
Post a Comment