TANGAZO


Tuesday, December 17, 2013

Rais wa Zanzibar, Dk. Shein azindua Kituo cha Afya Kajengwa, Makunduchi Unguja

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kufungua kituo cha Afya cha Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo, katika shamrashamra  za kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. (Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa Daktari dhamana Wilaya ya Kusini (DMO), Daniel Francis Pius (katikati), baada ya kukifungua kituo cha Afya cha Kijiji cha Kajengwa Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja leo, katika shamra shamra  kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Wasoma Utenzi Amina Makame Omar na Marium Amour Haji, kutoka Shehia ya Kijini, walipokuwa wakitoa burudani hiyo kwa wananchi wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katibu wa Kamati ya Maendeleo Shehia ya Kajengwa Makunduchi Nassor Simba, alipokuwa akisoma risala ya wananchi wa Kijiji hicho, wakati wa  ufunguzi wa  kituo cha Afya cha Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja leo, katika shamrashamra za kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wa Shehia ya Kijiji cha Kajengwa Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja na Vijiji vya jirani wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, alipokuwa akizungumza nao wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Afya kijijini hapo, katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Dk. Saleh Mohamed Jidawi, alipokuwa akitoa Taarifa na shukurani kwa  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, baada ya kukifungua kituo cha Afya cha Shehia ya Kajengwa  Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja leo, katika shamrashamra  kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo cha Afya Kajengwa Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja, wakiwa katika sherehe za ufunguzi wa kituo hicho, katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Sherehe hizo, zimefanyika leo na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa ni mgeni rasmi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja leo, wakati wa sherehe za ufunguzi wa Kituo cha Afya katika maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment