TANGAZO


Tuesday, December 17, 2013

Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wapigwa msasa kuhusu Changamoto za Milenia na Mkakati wa Matokeo Makubwa sasa

Mtaalamu wa mipango wa shirika la maendeleo la umoja wa mataifa hapa nchini, UNDP, Amon Manyama (kulia), akifungua warsha ya siku moja  moja iliyoandaliwa na ofisi ya bunge kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP), chini ya mpango wake wa usaidizi wa shughuli za bunge, mjini Dodoma jana. Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa wabunge, ililenga kujadili mafanikio na changamoto za mpango wa serikali wa kupambana na umasikini (MKUKUTA), changamoto za millennia na mkakati wa serikali wa hivi karibuni wa “Matokeo Makubwa Sasa” na umuhimu wake kwa jamii. Katikati ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii, Margareth Sitta na Mkurugenzi wa kuondoa umasikini wizara ya fedha, Anna Mwasha

Mbunge wa Karagwe, Gozbert Blandes, akichangia mada mbalimbali zilizowasilishwa na wataalamu kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ofisi ya bunge kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP), chini ya mpango wake wa usaidizi wa shughuli za bunge, mjini Dodoma jana. Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa wabunge, ililenga kujadili mafanikio na changamoto za mpango wa serikali wa kupambana na umasikini (MKUKUTA), changamoto za millennia na mkakati wa serikali wa hivi karibuni wa “Matokeo Makubwa Sasa” na umuhimu wake kwa jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya bunge ya Huduma za Jamii, Margareth Sitta, (Kulia), akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na ofisi ya bunge kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP), chini ya mpango wake wa usaidizi wa shughuli za bunge, mjini Dodoma jana. Warsha hiyo iliyoandaliwa kwa wabunge, ililenga kujadili mafanikio na changamoto za mpango wa serikali wa kupambana na umasikini (MKUKUTA), changamoto za millennia na mkakati wa serikali wa hivi karibuni wa “Matokeo Makubwa Sasa” na umuhimu wake kwa jamii. Kushoto ni mtaalamu wa mipango wa UNDP hapa nchini, Amon Manyama.
 Msasa ukiendelea ...

No comments:

Post a Comment