Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumatatu, Desemba 30, 2013, amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini.
\
Taarifa
iliyotolewa usiku wa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue inasema
kuwa Kamishna Mangu anachukua nafasi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini
anayestaafu, Saidi Mwema.
Kabla
ya uteuzi wake unaoanza keshokutwa, Januari Mosi, 2014, Kamishna Mangu alikuwa
Mkurugenzi wa Inteligensia ya Jinai (Director of Criminal Intelligence)
katika Jeshi hilo la Polisi.
Aidha,
taarifa hiyo inasema kuwa Rais Kikwete amemteua Kamishna Abdulrahman Kaniki
kuwa Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambayo ni nafasi mpya katika muundo wa sasa
wa Jeshi la Polisi.
Kabla
ya uteuzi wake, Kamishna Kaniki alikuwa Kamishna wa Uchunguzi wa Kijinai (Commissioner
for Forensic Investigations).
Mkuu
wa Jeshi la Polisi mpya ataapishwa kesho, Jumanne, Desemba 31, 2013 katika Viwanja vya Ikulu,
Dar es Salaam.
Imetolewa na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar
es Salaam.
30
Desemba, 2013
No comments:
Post a Comment