Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto, Bi. Pili Dumea akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mzunguko wa sita tuzo kwa mashindano ya uandishi wa riwaya za kingereza, kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi.
Pili Dumea akionesha kitabu cha Run Free cha mshindi wa kwanza wa tuzo za Burt katika
mzunguko wa tano kilichoandikwa na Richard Mabala, kushoto ni Mratibu wa tuzo
hizo Bw. Ramadhan Ali.Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akionesha kitabu cha The Birthday Party cha mshindi wa pili wa tuzo za Burt katika mzunguko wa tano kilichoandikwa na Mukama Mwijarubi, kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea akionesha kitabu cha Tears from a Lovely Heart cha mshindi wa tatu wa tuzo za Burt katika mzunguko wa tano kilichoandikwa na Israel Yohana, kushoto ni Mratibu wa tuzo hizo Bw. Ramadhan Ali.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mzunguko wa sita tuzo kwa mashindano ya uandishi wa riwaya za kingereza.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji toka Mradi wa Vitabu vya Watoto Bi. Pili Dumea (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa mzunguko wa sita tuzo kwa mashindano ya uandishi wa riwaya za Kiingereza.
Na Kiza Sungura-MAELEZO-Dar es Salaam
Mradi wa vitabu vya watoto Tanzania umezindua shindano la uandishi wa riwaya za Kiingreza
kwa ajili ya kuwajengea msingi wa kujifunza kwa urahisi lugha hiyo vijana hapa
nchini.
Shindano hilo ni sehemu ya tuzo ya Burt ya fasihi ya
kiafrika iliyoanza kutekelezwa tangu mwaka 2008 na kwa mwaka huu ni mzunguko wa
sita wa mashindano ya uandishi wa riwaya za kiingereza kwa ajili ya vijana .
Akizindua shindano hilo leo(jana) jijini Dar e
salaam Katibu Mtendaji wa Mradi huo Bibi Pilli Dumea amesema kuwa lengo la mashindano hayo ni kuatambua kazi
nzuri zinazofanywa na waandishi wa fasihi barani Afrika na kuwahamasisha
waandishi wachanga waweze kushiriki katika ujenzi wa fasihi .
“Lengo la mashindano haya ni kutoa changamoto kwa
waandishi na wasomaji wa riwaya za
kiingereza wa hapa nchini na Afrika kwa ujumla ili kuongeza kasi ya usomaji na uandishi wa riwaya za kiingereza ili
kuongeza uelewa wa lugha hiyo”, alisema
Bibi. Pilli.
Aidha aliongeza kuwa mashindano haya yatakuwa na
ushindani mkubwa kwani yanashirikisha washiriki toka nchi nne ambazo ni wenyeji
Tanzania, Ethiopia, Ghana pamoja na
Kenya.
“Mashindano haya ya mzunguko wa sita yatakuwa na
ushindani sana na zawadi ya mzunguko huu ni dola za kimarekani elfu tisa kwa
mshindi wa kwanza, dola elfu saba kwa mshindi wa pili na dola elfu tano kwa
mshindi wa tatu”, aliongeza Bibi Pilli.
Alisema kuwa mwisho wa kupeleka muswada wa riwaya itakuwa
mwakani Mwezi Mei na muswada huo unatakiwa uwe na maneno yasiyozidi elfu 20 na
yasizidi elfu 40.
Muswada huo unatakiwa uwasilishwe kwa Mradi wa
Vitabu vya Watoto Tanzania katika barua pepe yao ya childrensbook@gmail.com
au nakala katika ofisi zao.
No comments:
Post a Comment