Kumekua na mapigano makali ya kurushiana risasi na silaha nzito
nzito katika mji wa Bangui nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati saa moja kabla
Baraza kuu la Umoja wa Mataifa halijapitisha azimio la kupeleka majeshi ya
kutoka Afrika na Ufaransa.
Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache.
Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
No comments:
Post a Comment