Nchini Burundi vuta nikuvute kati ya serikali na baadhi ya
vyama vya upinzani kuhusu marekebisho ya vipengee vya katiba inazidi
kutokota.
Vyama hivyo vya upinzani vimetishia kuandaa maandamano makubwa wiki ijayo
kupinga marekebisho hayo.Mageuzi hayo ambayo serikali inasema sio jambo kubwa, yamekosolewa na wakosoaji wake wakisema kua huenda yakafufua mgogoro wa kikabila ambao ndio ulikuwa chanzo cha vita katika nchi hiyo ndogo ambayo iliwahi kukumbwa na tatizo la makundi ya waasi kuhangaisha taifa.
Wakosoaji pia wanasema kuwa hii ni njama ya Rais Pierre Nkurunziza kutaka kusalia mamlakani kinyume na sheria.
Ikiwa katiba itafanyiwa mageuzi, huenda kikwazo cha kupitisha sheria bungeni kikalegezezwa na kuhitaji tu idadi kubwa ya wabunge wala sio thuluthi mbili ya wabunge kuhalalisha sheria kama ilivyo sasa.
Hatua kama hii itawapa uhuru mkubwa wabunge wa kabila la Hutu ambao ndio wengi bungeni uwezo mkubwa wa kupitisha sheria.
Wabunge wa Tutsi wanashikilia asilimia 40 ya viti vya bunge.
Mageuzi hayo pia yatampunguzia mamlaka makamu wa kwanza wa Rais ambaye sharti atoke chama au kabila tofauti na Rais, na pia kitapunguzia baraza la Senate mamlaka ya kuhakikisha kazi za serikali zinagawanya visawasawa kati ya makabila yote.,
Rais Pierre Nkurunziza, ambaye ni Mhutu anaongoza chama cha (CNDD-FDD), wakati makamu wake Bernard Busokoza ni mtutsi kutoka chama cha UPRONA.
No comments:
Post a Comment