Baba mtakatifu Papa Francis ameidhinisha kamati ya Vatican
itakayopambana na visa vya unajisi wa watoto katika kanisa katoliki pamoja na
kuwasaidia waathiriwa kwa kuwapa ushauri nasaha.
Tangazo hili limelotolewa na naibu askofu mkuu Sean O'Malley mjini Boston
Marekani, na linakuja baada ya kufanyika mkutano kati ya Papa na makadinali wake
wanane ambao humshauri.Papa Francis, amesema kuwa swala la kukabiliana na visa vya makasisi kuwanajisi watoto ni muhimu sana ili kuweza kulirejeshea hadhi kanisa Katoliki.
Kadinali, Sean O'Malley, naibu askofu mkuu wa kanisa hilo mjini Boston, alisema kuwa kamati hiyo inaweza kutoa mwongozo wa kikazi kwa makadinali na maafisa wa kanisa ili kulainisha utenda kazi wa viongozi wa kanisa.
Mji wa Boston ndio ulikuwa kitovu cha madai ya makasisi kuwanajisi watoto nchini Marekani mwaka 2002.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, naibu Askofu alisema kuwa kamati hiyo mpya ilipendekezwa na baraza la makadinali, ambalo lilibuniwa ili kufanyia mageuzi kanisa katoliki. Papa aliliidhinisha Alhamisi.
No comments:
Post a Comment