Baadhi ya
waokoaji wa jeshi la zimamoto wakiwa
katika zoezi la uzimaji wa moto wa
ndege Nov. 21,2013 katika eneo maalumu
kwa ajili ya zoezi hilo jijini Dar es
Salaam.Mazoezi hayo yamewashirikisha
wanafunzi 22.
Baadhi ya waokoaji wa jeshi la zimamoto wakiwa katika zoezi la uzimaji wa moto wa ndege Nov. 21,2013 katika eneo maalumu kwa ajili ya zoezi hilo jijini Dar es Salaam.Mazoezi hayo yamewashirikisha wanafunzi 22.Baadhi ya Askari wahitimu wa Jeshi la zimamoto nchini wakifanya zoezi la kumkimbiza majeruhi kumpeleka hospitali baada ya kumuokoa kwenye ajali.zoezi hilo limeshuhudiwa na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh.Dkt.Emannuel Nchimbi.(hayupo katika picha) Nov.21,2013 jijini Dar es Salaam.
Naibu Kamishna Jenerali wa jeshi la Zimamoto Tanzania Luteni Kanali Lidwino Mgumba akitoa taarifa ya mafunzo ya kozi ya zoezi la kuzima moto wa ndege Nov. 21,2013 jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Askari wa Jeshi la zima moto waliomaliza mafunzo ya kuzima moto wa ndege wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo katika picha), Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, Nov, 21,2013. Wahitimu hao katika risala yao, wamesema kwamba wamepata uelewa mkubwa utakaowawezesh a kufanya majukumu yao kikamilifu, ikiwemo kuzima moto, kuokoa watu na kulinda mali zao.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto) akimpongeza Protacy Lichenjele(kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha uaminifu,kwani kitendo cha askari huyo kurudisha fedha baada ya kugundua amezidishiwa ni kitendo chenye kuhitaji moyo na uzalendo wa kuigwa.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi(kulia), akipongezana na Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto nchini Piusi Nyambacha (kushoto) baada ya kumalizika hafla ya kozi ya zoezi la kuzima moto wa ndege kwa askari wa jeshi la zima moto, jana Nov.21,2013 jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Mwanakombo Jumaa)
No comments:
Post a Comment