TANGAZO


Friday, November 22, 2013

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akutana na wadau wa Mradi wa "Power Afrika wizarani kwake, pia amekutana na Balozi wa Uturuki nchini

Ofisa kutoka Wizarani anayeshughulikia masuala ya Mradi wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bi .Wanja Mtawazo akiteta jambo na wadau wa Power Africa, walipofika Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Asteria Muhozya- Wizara ya Nishati na Madini.)
Bibi Oren E Whyche-Shaw, Ofisa Mshauri wa masuala ya Utawala wa Shirika la USAID, akielezea jambo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia), wakati wa kikao hicho jijini leo.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini, wakifuatilia kikao kati ya Waziri wa Nishati na Madini na wadau wa Mradi wa Power Africa katika kikao hicho jijini leo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akisisitiza jambo, wakati alipokutana na wadau wa Mradi wa Power Africa, kujadiliana juu ya hali halisi ya Utekelezaji wa Mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini, Sospter Mhongo akizungumza na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Ali Davutoglu, alipomtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, kujadiliana kuhusu masuala ya uwekezaji nchini.

No comments:

Post a Comment