Kaimu Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt. Hamza Kabelwa akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) mikakati ya Serikali katika kuendeleza huduma za hali ya hewa katika sekta ya usafiri wa baharini,Visiwani Zanzibar na katika maziwa nchini,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka hiyo Bi.Monica Shayo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu toka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dkt. Hamza Kabelwa akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) cheti cha utambuzi walichopokea kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini(ZMA) kutokana na kuutambua mchango wao katika usafiri wa Baharini.Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bi. Georgina Misama.
KATIKA
jitihada za kupunguza maafa na kuhakikisha kuwa huduma za hali ya hewa nchini
zinazidi kuwa bora, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imefungua kituo cha huduma
za hali ya hewa kwa watumiaji wa usafiri wa baharini. Ofisi hiyo ilianzishwa
rasmi tarehe 28/04/2013 katika bandari ya Zanzibar, ikiwa na lengo la
kuhakikisha taarifa za hali ya hewa kwa usafiri wa baharini zinapatikana na
ushauri unatokewa kwa watumiaji kwa wakati, hapo awali huduma hizi zilikuwa
zinaandaliwa na kutolewa kutoka ofisi za hali ya hewa zilizopo kituo kikuu cha
utabiri – Dar es Salaam na uwanja wa ndege wa Karume - Zanzibar.
Kwa upande wa usafiri katika maziwa, Mamlaka
imenunua mtambo mkubwa wa kuchambua taarifa za hali ya hewa (computer cluster)
utakaowezesha huduma za hali ya hewa kutolewa katika maziwa yote makuu hapa
nchini.
Katika
kutambua mchango mkubwa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri Baharini (ZMA), iliipatia Mamlaka
ya Hali ya Hewa cheti cha kuutambua mchango huo (Certificate of Appreciation)
kwa kutambua mchango wa Mamlaka katika usafiri wa baharini.
Vilevile,
Mamlaka kupitia ofisi ya Zanzibar ilitunikiwa cheti cha kuutambua mchango wake
katika kukabiliana na maafa (Certificate of Appreciation). Cheti hicho
kilitolewa na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais SMZ, Kitengo cha Maafa.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
No comments:
Post a Comment