Na Neema Mgonja, DODOMA
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, amefunguka na kusema kuwa hakuna haja ya kuendeleza mabishano na nchi jirani na badala yake mbali na hilo, Lowassa pia alisema anaishangaa Serikali kwa kutokuwa na maamuzi magumu na badala yake imebaki kulalamika juu ya mambo mbalimbali na kuongeza kuwa anahitajika mtu wa kuweza kufanya maamuzi hayo kwa maslahi ya Taifa.
Mbunge wa Monduli Edward Lowassa |
"Tusigombane na kina Kagame na hao akina Uhuru na Museveni hakuna haja ya kufanya hivyo kama wao wamekwenda Sudani Kusini sisi twende East Congo, ambapo ni kuzuri zaidi, sisi twaweza kufufua Reli ya Kati na kwenda Congo tukafanikiwa zaidi yao, " alisema Lowassa.
Kuhusiana na Serikali kutochukua maamuzi magumu, Lowassa alisema inashangaza kuona Serikali ikiendelea kulalamika badala ya kuchukua maamuzi magumu.
"Tatizo moja la nchi hii, mnazungumza mambo hakuna utekelezaji, tofauti na nchi za wenzetu hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, kinatakiwa chombo kinachofanya utekelezaji".
"Haiwezekani kila mtu akawa analalamika lalamika tu, Serikali inalalamika kila mtu analalamika lazima awepo mtu mmoja wa kufanya maamuzi magumu," alisema Lowassa.
Lowassa aliongeza kuwa kamwe mipango ya taifa haiwezi kutekelezeka kutokana na kuwa na vipaumbele vingi ambavyo havikamiliki.
Lowasa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema kuwa ni vyema Serikali ingekuwa na mipango michache ambayo inatekelezeka na yenye tija ambayo ndiyo ingestahili kupewa kipaumbele katika utekelezaji wake.
Alivitaja vipaumbele ambavyo alisema angekuwa yeye angeliviweka na kusimamia utekelezaji wake kama angekuwa kiongozi na kusema kipaumbele kikubwa kingelikuwa ajira.
Alivitaja vipaumbele vingine ambavyo angevisimamia yeye kama angelikuwa kiongozi ni pamoja na Elimu na Ujenzi wa Reli ya kati.
"Lazima tuangalie suala la ajira ni muhimu sana, hili ndilo pendekezo langu la kwanza, kipaumbele cha pili ni elimu, tuangalie jamani mjadala wa elimu tusiupuuze.
"Hizi hatua zinazochukuliwa chukuliwa hazipendezi, mimi nilitegemea tutapata ufumbuzi, haitoshi kuchukua wanafunzi wengi wakimaliza digirii hazina kazi, aiana ya elimu tunayotoa aina msaada".
Lowassa aliongeza kuwa; "Kelele zinazopigwa na wananchi zisipuuzwe tufanye mjadala na wananchi, tuzungumze tatizo liko wapi, tuwasahidie vijana wetu katika kujikwamua kielimu"alisema
Lowassa
Mbali na hilo Lowasa alisema kuwa Tanzania inakosa kiongozi ambaye ni jasiri wa kufanya maamuzi ambayo ni sahihi na magumu.
“Tatizo ni kuwa mipango inayopangwa ni
mingi lakini haitekelezeki na hiyo inatokana na kukosekana kwa kiongozi
ambaye anaweza kusimamia
kikamilifu"
“Viongozi wanavijika kuwa na maamuzi lakini badala yake inabaki kuwa kuwa na ubabaishaji ambao hauna maamuzi magunu ya kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuleta tija”alisema Lowasa.
Akizungumzia suala la barabara Lowasa
alisema kuwa pamoja na serikali kutengeneza barabara kwa kiwango cha
lami lakini barabara hizo zinaharibika kila siku tofauti na inavyostahili.
Alisema kuwa ni muhimu suala la foleni Dar es Salaam likatazamwa kwa makini, kwakuwa linachangia kupunguza nguvu kazi za watu.
"Foleni Dar es Salaam nakupongeza Mwakyembe, anajitahidi 'keep it up', lakini
haitoshi, Serikali haiwezi kukaa hivi
hivi, hii ni tatizo watu wanapoteza muda mwingi sana lazima ufumbuzi wa
makini," alisema Lowassa.
No comments:
Post a Comment