Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Symbion, Peter Gathercole (kulia) akifafanua jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-Salaam, alipokutana na Uongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuelezea mikakati ya Maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni wajumbe alioongozana nao.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonard Thadeo (kushoto) akielezea jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-Salaam, wakati uongozi wa Wizara ulipokutana na Ujumbe wa Viongozi wa kampuni ya Symbion ya Marekani Kujadili Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Henry Lihaya na Afisa Michezo Mkuu, Charles Yasse Mattoke
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Ndugu. Leonard Thadeo (kushoto) akielezea jambo, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-Salaam, wakati uongozi wa Wizara ulipokutana na Ujumbe wa Viongozi wa kampuni ya Symbion ya Marekani Kujadili Maandalizi ya Ujenzi wa Kituo Kikubwa cha Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Tanzania (BMT), Henry Lihaya na Afisa Michezo Mkuu, Charles Yasse Mattoke.
Viongozi wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wakiwa katika mazungumzo na Ujumbe wa Viongozi wa Kampuni ya Symbion ya Marekani walipokutana, leo Novemba 5, 2013, jijini Dar-es-Salaam kujadili maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Maendeleo ya Mchezo wa soka nchini (Soccer Academy), pamoja na viwanja vya michezo (sports courts). (Picha zote na Johary Kachwamba-MAELEZO) |
No comments:
Post a Comment