TANGAZO


Tuesday, November 5, 2013

Miili ya waandishi yawasili Ufaransa



Rais Francois Hollaned alikuwa miongoni mwa wale waliokuwa katika uwanja wa ndege kuipokea miili hiyo.
Miili ya waandishi wa habari wa Ufaransa waliouawa Kaskazini mwa Mali, imepelekwa mjini Paris.
Ghislaine Dupont mwenye umri wa miaka 57 na Claude Verlon mwenye umri wa miaka 58, walikuwa wanafanya kazi na kituo cha Radio cha shirika la habari la Ufaransa, walitekwa nyara na kuuawa siku ya Jumamosi baada ya kumuhoji kiongozi mmoja mjini Kidal.
Mwenzake wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita,aliapa kufanya kila awezalo kuwakamata watu waliohusika na mauaji hayo.Rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa miongoni mwa watu waliofika katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle kuipokea miili hiyo.
Miili ya wawili hao, ilisafirishwa hadi katika uwanja wa ndege wa Bamako Jumapili usiku.
Miili yao ilisindikizwa na wafanyakazi wenzao katika barabara za Bamako kwa kimya kikuu.
Aidha walipokewa na jamaa zao wakiandamana na rais Hollande pamoja na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Laurent Fabius.
Bwana Fabius ametaja mauaji hayo kama mauaji mabaya sana ya kupangwa.
Mnamo siku ya Jumatatu , polisi nchini Mali walisema kuwa washukiwa kadhaa wa mauaji hayo, wamekamatwa

No comments:

Post a Comment