Pesa zinazotumwa nchini Somalia kupitia Dahabshiil zinafika pauni bilioni moja kila mwaka
Jaji mmoja nchini Uingereza ameiagiza benki ya Barclays kutofunga huduma moja ya kutuma pesa inayotumiwa kutuma mamilioni ya dola nchini Somalia kila mwaka.
Agizo hilo la mda lilitolewa hadi uamuzi kamili wa kesi utakapotolewa mnamo mwaka ujao na kuwa afueni kwa watumiaji wa huduma hiyo kwani wataendelea kutuma pesa kwa muda .
Kampuni ya kutuma pesa ya Dahabshiil ambayo ni moja ya kampuni kubwa zaidi barani Afrika zinzotoa huduma hiyo, inadai kuwa benki ya Barclays inatumia fursa ya nafasi yake kubwa kuiponda.
Lakini benki hiyo imejitetea ikisema kuwa inajiweka katika hali ya kupigwa faini kubwa kwa kuwa fedha hizo zinatumwa katika eneo la hatari.
Barclays ilipanga kukatiza huduma hiyo kutokana na wasiwasi wake kuwa kampuni hiyo inafanya biashara haramu ya kutengeza pesa.
Shirika la misaada la Oxfam limesema kuwa suluhu ya mda mrefu inatakikana ili kuhakikisha kuwa raia wa Somalia wanapata chakula ,dawa na elimu.
Dahabshiil ndio kampuni kubwa zaidi ya inayotoa huduma ya kutuma pesa kwa njia ya elektroniki inayotumiwa na wasomali lakini moja wanaoishi nchini Uingereza.
Wasomali hao hutumia huduma hiyo kutuma mamilioni ya pauni kila mwaka kwa marafiki na jamaa zao nchini Somalia, ikiwa huduma muhimu sana kwa taifa hilo ambalo linakumbwa na mgogoro wa miaka mingi w akisiasa.
Mahakama ilitoa uamuzi wake na kuipa afueni ya muda kampuni ya Dahabshiil ambayo hutumia Barclays katika kutoa huduma zake hadi kesi itakapokamilika.
"huu sio ushindi tu kwa Dahabshiil. Ni ushindi kwa mamilioni ya wasomali na waafrika wengine wengi ambao maisha yao yanategemea huduma hizo,'' ilinukuu taarifa ya Dahabshiil
Lakini shirika la misaada la Oxfam limeonya kuwa uamuzi huo wa mahakama ni wa muda tu, ikisema kuwa hii sio suluhisho la kudumu la tatizo na kwamba suluhu la kudumu linahitajika ili kuweka salama maisha ya mamilino nchini Somalia wanaotegemea huduma hiyo kwa mahitaji ya elimu, dawa na chakula.
No comments:
Post a Comment