RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa
Serikali imedhamiria kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao
la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Aidha, Rais Kikwete
amesema kuwa ni muhimu kwa Serikali kuchukua hatua za kukabiliana na tatizo la
minazi kwa sababu watu wengi katika baadhi ya maeneo ambayo uchumi wake
unategemea zao la mnazi wanakabiliwa na hatari ya kweli kweli ya kuathirika kwa
maisha yao.
Rais Kikwete ametoa
uhakikisho huo jana, Jumamosi, Novemba 16, 2013, wakati alipokutana na Waziri wa
Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa
Jagath Pushpakumara na ujumbe wake mjini Colombo. Waziri huyo aliandamana na
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti ya Minazi ya Sri Lanka.
Rais Kikwete yuko
nchini Sri Lanka kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuia ya
Madola (CHOGM) unaomalizika leo, Jumapili, Novemba 17, 2013. Mkutano huo wa siku
tatu, ulianza juzi, Ijumaa, Novemba 15, 2013.
Mheshimiwa
Pushpakumara na ujumbe wake walikuwa wanamwelezea na kumkabidhi Rais Kikwete
Ripoti ya Magonjwa ya Minazi iliyoandaliwa na wataalam wa minazi wa Sri Lanka
ambao walitembelea Tanzania Julai mwaka huu.
Wataalam hao
walitembea Tanzania na kufanya utafiti kuhusu ugonjwa unaolikabili zao la minazi
kufuatia ahadi ya Rais Mahinda Rajapaksa aliyoitoa kwa Rais Kikwete wakati
alipofanya ziara rasmi ya Tanzania Juni 27, 2013, na baadaye kushiriki katika
Mkutano wa Smart Partnership Juni mwaka huu.
Rais Rajapaksa alitoa
ahadi hiyo baada ya kuelezwa na Rais Kikwete kuhusu zao la kukauka kwa minazi
nchini. Mnazi ni zao muhimu sana katika uchumi wa Sri Lanka na ni zao tegemeo
kwa wananchi wa Taifa-Kisiwa hilo kilichoko kusini mashariki mwa India katika
Barahri ya Hindi.
Wataalamu waliofuatana
na Waziri huyo wamemwambia Rais Kikwete kuwa ugonjwa unaolikabili zao hilo la
minazi ambao pia unashambulia minazi katika eneo la Caribbean hauna tiba kwa
sababu mpaka sasa hakuna taasisi yoyote ya utafiti imegundua dawa
hiyo.
Wataalam hao ambao
walikaa Tanzania kwa wiki moja, zikiwamo siku mbili katika Zanzibar, wanasema
kuwa zao hilo la mnazi, kama ilivyo katika nchi nyingine zinazolima zao hilo,
lina uwezo mkubwa wa kusaidia uchumi kupitia viwanda vidogo vidogo.
Wakati wakiwa Tanzania, wataalam hao wa Sri Lanka
walifanya uchunguzi na utafiti kwa karibu na wataalam wa Taasisi ya Utafiti ya
Kilimo ya Mikocheni (MARI).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (shati jeupe) na ujumbe
wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko. (Picha zote na Ikulu)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi inayotokana na zao la mnazi toka kwa Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (kushoto) na ujumbe wake mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.
Picha ya pamoja ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, wakati alipokuwa na Waziri wa Maendeleo ya Minazi na Maendeleo ya Shamba la Janatha wa Sri Lanka, Mheshimiwa Jagath Pushpakumara (kulia kwa Rais) na ujumbe wake, mjini Colombo, Sri Lanka, kuzungumzia njia za kushirikiana kukabiliana na maradhi ya mazao, likiwamo zao la mnazi ambalo linakabiliwa na tatizo la mnyauko.

No comments:
Post a Comment