TANGAZO


Sunday, November 17, 2013

Mapigano ya kikabila yaua 100 Sudan

 

Raia wa Sudan waliokimbia makazi yao kwa sababu ya machafuko

Habari kutoka Sudan zinasema mapigano makali ya kikabila kati ya makabila mawili kwenye mpaka wa jimbo la Mashariki mwa Darfur yamesababisha vifo vya zaidi ya watu mia moja katika siku za hivi karibuni.
Radio ya taifa imeripoti kutokea kwa mapigano siku ya jumamosi kati ya kabila la Messeriya ambalo linapambana na kabila la Salamat katika eneo la kusini magharibi la Umm Kukhun.

Taarifa nyingine zinasema askari wa Chad waliokuwa wakifanya doria na majeshi ya Sudan katika mpaka baina ya nchi hizo mbili ni miongoni mwa waliojeruhiwa.
Umoja wa mataifa umeonya kuwa mapigano hayo ya kikabila baina ya makabila hayo mawili yamesababisha maelfu ya raia kukimbia makazi yao katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment