TANGAZO


Wednesday, November 13, 2013

Rais Kikwete aifariji familia ya marehemu Dk. Mvungi

*Tume ya Mabadiliko ya Katiba yatoa taarifa ya kuwasili kwa mwili wa marehemu, Dk. Mvungi

Rais Jakaya Kikwete akitiasaini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dk. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba, jijini Dar es Salaam leo. 
Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete  wakiifariji familia ya Marehemu Dk. Sengondo Mvungi (Picha na Freddy Maro)
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akitiasaini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa tume hiyo, Dk. Sengondo Mvungi nyumbani kwake, Kibamba jijini Dar es Salaam leo.
Rais JakayaKikwete (katikati), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto), nyumbani kwa marehemu Dk. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia na Mjumbe wa Tume, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim. 
MjumbewaTumeyaMabadilikoyaKatiba Richard Lyimoakimpa pole mkewamarehemuDkt. SengondoMvungi, Bi. Anna MvungiwakatiWajumbewaTumewalipokwendakumpa pole. 
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi alipokwenda kumpa pole nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Jaji Joseph Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim (kulia), walipokutana nyumbani kwa marehemu, Dk. Sengondo Mvungi, Kibamba jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Tume ya Katiba)

Na Omega Ngole,
Jumatano, Novemba 13, 2013 
TUME ya Mabadiliko ya Katiba inawafahamisha wananchi kuwa taratibu za kuusafirisha mwili wa Mjumbe wake, Dk. Sengondo Mvungi aliyefariki nchini Afrika Kusini zimekamilika na mwili wake unatarajia kuwasili nchini siku ya Ijumaa, Novemba 15, 2013.

Baada ya kuwasili, mwili huo,  utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo, iliyopo jijini Dar es Salaam.

Aidha, siku ya Jumamosi, Novemba 16, 2013 kutafanyika Ibada ya mazishi katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi. Baada ya misa, marehemu ataagwa katika Viwanja vya Karimjee kuanzia saa 6:30 mchana siku hiyohiyo ya Jumamosi, Novemba 16, 2013.
Aidha, Marehemu Dkt. Mvungi anatarajiwa kusafirishwa siku ya Jumapili, Novemba 17, 2013 kwenda Kisangara Juu, Wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika siku ya Jumatatu, Novemba 18, 2013.

Dkt. Mvungi alifariki jana (Jumanne, Novemba 12, 2013) katika Hospitali ya Millpark jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini, alikopelekwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi akitokea Kitengo cha Mifupa Muhimbili (MOI) aliokuwa amelazwa baada ya kuvamiwa nyumbani kwake Kibamba, wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam na watu waliomjeruhi vibaya kichwani usiku wa kuamkia siku ya Jumapili, Novemba 3, 2013.

Wakati huohuo, Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba leo (Jumatano, Novemba 13, 2013), wameungana na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kufika nyumbani kwa marehemu Dk. Mvungi eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa pole kwa familia, ndugu na jamaa wa marehemu, Dk. Mvungi.

No comments:

Post a Comment