TANGAZO


Wednesday, November 13, 2013

Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kukabiliana na tatizo la Ujangili nchini

Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dorina makaya akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mikakati ya Wizara hiyo, katika kukabiliana na tatizo la ujangili nchini ikiwa ni pamoja na kushirikisha wadau mbalimbali katika harakati hizo, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari, Maelezo, Bi. Zamaradi Kawawa. (Picha zote na Eliphace Marwa-Maelezo)
Mwanaharakati wa kutetea haki za wanyama  nchini Mchungaji Clement aloyce akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu umuhimu wa wananchi kushiriki katika uhifadhi wa wanyama pori, hasa tembo ambao wapo katika hatari kutokana na ujangili unaofanywa dhidi ya wanyama hao, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Wanyama Pori Mkuu toka Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. John muya.

No comments:

Post a Comment