Baadhi ya waandishi wa habari, wakiwa kazini wakati Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, alipokuwa akizungumza nao, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kushoto ni Kaimu Msemaji wa ofisi hiyo, Augustino Tendwa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kulia ni Ofisa habari wa Idara ya Habari, Maelezo, Fatma Salum.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kushoto ni Kaimu Msemaji wa ofisi hiyo, Augustino Tendwa. Fatma Salum-Maelezo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kushoto ni Kaimu Msemaji wa ofisi hiyo, Augustino Tendwa. Fatma Salum-Maelezo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Uwekezaji na Uwezeshaji, Ofisi ya Waziri Mkuu, John Mboya (katikati), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu Utaratibu wa Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi. Kushoto ni Kaimu Msemaji wa ofisi hiyo, Augustino Tendwa na kulia ni Ofisa habari wa Idara ya Habari, Maelezo, Fatma Salum.
1.0UTANGULIZI
Maana
ya Dhana ya PPP na Uzoefu wa Kimataifa
Ndugu
Wanahabari, Dhana hii ya Ubia baina ya Sekta ya Umma
na Sekta Binafsi inahusisha mikataba baina ya sekta ya umma na sekta binafsi
ambapo sekta binafsi inahusika na kukarabati, kujenga, kuendesha, kutunza, au
kusimamia mradi mzima au sehemu yake kulingana na vigezo maalum vya utendaji
vilivyowekwa na sekta ya umma. Kwa utaratibu huu, sekta binafsi inabeba kwa
kiasi kikubwa utekelezaji wa uwekezaji huo kwa muda fulani, kwa mategemeo ya
kupata faida na malipo kulingana na mkataba husika. Kwa mfano, Serikali inaweza
kuwa na mkataba na mwekezaji kujenga barabara yenye urefu wa km. 100 na yenye
viwango fulani; na mwekezaji atatakiwa kusanifu, kujenga, kuendesha kwa gharama
zake na hatimaye baada ya kurudisha mtaji wake na faida, anakabidhi mradi huo Serikalini.
Kimsingi ubia wa aina hii ni njia
muafaka inayoweza kutatua matatizo yanayotokana na ukosefu
wa fedha kuwezesha Serikali kusimamia, kuendesha na kutunza rasilimali za umma kwa ufanisi. Faida za utaratibu wa PPP ni
pamoja na kupunguza mzigo kwenye bajeti ya Serikali kutokana na kutumia ujuzi
na ufanisi wa mwekezaji, hivyo kuiwezesha Serikali kuelekeza Raslimali zake
kwenye miradi mingine ambayo utaratibu wa ubia hauwezekani.
Katika utaratibu wa PPP,
Sekta Binafsi inabeba kwa kiasi kikubwa gharama zinazohusiana na ujenzi na
uendelezaji wa mradi. Aidha, miradi tunayozungumzia hapa siyo ubinafsishaji wa
mashirika ya umma ambapo Serikali inauza mali zake na Sekta Binafsi inakuwa na
jukumu la kuendesha kwa faida. Miradi ya PPP tunayozungumizia hapa ni ile
ambayo kimsingi ni jukumu la Serikali kuiendeleza, lakini kutokana na uchambuzi
wa kina inaonekana kuwepo na uwezekano wa wawekezaji kuwekeza kwa faida. Mifano
ya miradi hii ni kama vile ujenzi wa barabara, reli, viwanda vya ndege na
huduma za kijamii kama vile huduma za afya na elimu.
Mataifa mbalimbali kama
vile India, Malaysia, Korea, Marekani, Uingereza, Ujerumani, Australia, Chile,
Brazili, Afrika Kusini na Lesotho
yanatumia utaratibu huu kutekeleza miradi kama vile barabara za kulipia
(toll roads), usafiri wa reli, ujenzi na uendeshaji wa viwanja vya ndege,
huduma za maji, ujenzi wa magereza, huduma za afya n.k. Kwa mfano, kwa upande
wa Afrika Kusini na Lesotho wana
hospitali za kisasa na barabara za kulipia zinazoendeshwa kwa utaratibu
wa PPP.
2.
SERA YA UBIA BAINA YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI (2009)
Serikali yetu kama yalivyo
Mataifa mbalimbali inakabiliwa na changamoto za upatikanaji wa Raslimali za
kutosha za bajeti kuweza kutekeleza miradi na huduma za umma. Mwaka 2009 Serikali iliandaa Sera ya Ubia
baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi kwa lengo la kuweka mazingira wezeshi ya Kisera, Kisheria na Kitaasisi yenye lengo
la kutoa fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika ubia huo.
Sera inalenga kutoa
miongozo ya ujumla kuhakikisha kuwa kama Taifa tunaandaa na kutekeleza miradi
mizuri. Miongozo hii ni pamoja na mfumo wa sera mahususi, kisheria na
kitaasisi; upembuzi yakinifu unaozingatia
masuala ya kiufundi, kiuchumi na kijamii; upatikanaji wa raslimali kutekeleza
miradi ya PPP; mchakato wa ununuzi; mfumo wa mgawanyo wa vihatarishi (risk
allocation); majadiliano ya mikataba; fursa za uwekezaji na uhamasishaji;
kujenga ufahamu, kujenga uwezo na usambazaji wa teknolojia, utaratibu wa tozo,
miradi ya ubia kwenye maeneo ya pembezoni na jitihada za uwezeshaji.
3.SHERIA
YA UBIA BAINA YA SEKTA YA UMMA NA SEKTA BINAFSI YA MWAKA 2010
Katika kutekeleza Sera
hiyo, Serikali iliandaa Sheria ya Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi
ya mwaka 2010 ambayo imeweka mfumo wa kitaasisi wa utekelezaji wa miradi na
huduma za ubia, pamoja na taratibu muhimu za kuzingatiwa. Kimsingi, Sheria
imeanzisha Kitengo cha Uratibu wa miradi ya ubia chini ya Kituo cha Taifa cha
Uwekezaji ambacho kina jukumu la kupokea, kuchambua na kuratibu miradi ya Ubia
(PPP) kutoka kwenye Wizara, Idara, Wakala na Taasisi za Serikali. Aidha, Kitengo cha Fedha chini
ya Wizara ya Fedha kimeanzishwa kwa lengo la kuchambua masuala ya fedha kama
vile mgawanyo sahihi wa athari zinazoambatana na mradi na athari kwenye bajeti
ya Serikali. Mamlaka za Serikali zina jukumu kubwa la kufanya uchambuzi wa kina
kuainisha na kutekeleza miradi kwa utaratibu wa PPP na kuiwasilisha kwenye
Vitengo hivyo kwa ajili ya uchambuzi.
4. KANUNI ZA UBIA BAINA YA SEKTA YA
UMMA NA SEKTA BINAFSI YA MWAKA ZA MWAKA 2011
Kanuni za Ubia baina ya
Sekta ya Umma na Sekta Binafsi za mwaka 2011 ziliandaliwa ili kubainisha taratibu
mahususi za kuzingatiwa kuanzia utambuzi wa mradi, upembuzi yakinifu, mchakato
wa ununuzi kumpata mwekezaji mahiri, kuandaa mkataba wa mradi na utekelezaji.
Kimsingi Kanuni zinaeleza kwa kina vigezo vya kuzingatiwa kuhakikisha kuwa
miradi na huduma za ubia zinaandaliwa kwa umakini kwa kuzingatia vigezo vya Sheria
ya PPP.
Kanuni zimebainisha kuwa upembuzi
yakinifu wa mapendekezo ya miradi kutoka Sekta ya umma (solicited PPP
Proposals) utafanywa na Mamlaka za Serikali na upembuzi yakinifu wa mapendekezo
ya miradi inayoibuliwa na sekta binafsi itafanywa na sekta binafsi. Vigezo vya kuzingatiwa katika kuandaa
mapendekezo ya awali ya miradi hii pamoja na upitishwaji wake vimewekwa bayana.
Kanuni pia zimeweka taratibu za uwasilishwaji wa upembuzi yakinifu kutoka ngazi
ya Mamlaka za Serikali, Kitengo cha Uratibu hadi Kitengo cha Fedha. Aidha,
Kanuni zimeweka utaratibu wa kufuatwa katika masuala ya zabuni, majadiliano na
kusainiwa kwa mikataba.
4. Utekelezaji wa Sera ya PPP
4.1
Wizara na Mamlaka za Serikali zinaendelea na kuainisha na kufanya upembuzi
yakinifu wa miradi ya PPP. Naomba nieleze kwa kifupi baadhi ya miradi ambayo
Serikali inaendelea na maandalizi ya msingi ili itekelezwe kwa utaratibu wa
PPP:
(i)
Mradi wa Ujenzi wa barabara ya Dar es
Salaam-Chalinze (km 100) kuwa barabara ya haraka (Expressway) ambapo Wakala wa
Barabara amekamilisha uandaaji wa upembuzi yakinifu wa awali (Prefeasibility
Study).
(ii)
Mradi wa
Ujenzi wa Bandari Mpya ya Bagamoyo na Eneo Huru la Biashara (Portside
Industrial Area) ambapo Serikali inashirikiana na mwekezaji kutoka China - China
Merchant (Holding) International kutekeleza miradi hii. Serikali inaendelea na
majadiliano na mwekezaji ili miradi hii ilete tija na manufaa kwa Taifa.
(iii)
Mradi wa Ujenzi wa Gati
Nne (4) katika Bandari ya Mtwara
ambapo taarifa ya Upembuzi yakinifu imewasilishwa kwenye Kitengo cha
Uratibu. Makadirio ya awali yanaonyesha
mradi utagharimu dola za Kimarekani
milioni 219.
(iv)
Mradi mpya wa Bandari ya Mwambani ambapo taarifa ya
Upembuzi yakinifu inafanyiwa kazi. Makadirio
ya awali yanaonyesha kuwa mradi huu utagharimu dola za Kimarekani milioni 790.
Utekelezaji wa Sera ya PPP
unahitaji sana wadau kujengewa uwezo. Kazi hii inatekelezwa na Mamlaka za
Serikali na Sekta Binafsi. Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa na kutoa mafunzo kwa
maofisa 60 walioteuliwa kusimamia utekelezaji wa miradi ya PPP. Hapa niseme pia kuwa jambo la msingi ni
kwamba utaratibu wa PPP hauna njia za mkato kwa kukwepa hatua za msingi kama
vile kufanya uchambuzi wa kina.
Naomba nimalizie kwa
kusema kuwa Serikali inafanyia marekebisho Sheria ya PPP kwa lengo la
kuunganisha Vitengo vya PPP na kurahisisha michakato ya utekelezaji. Kama mlivyosikia, ushirikishwaji wa sekta
binafsi katika kutekeleza miradi hii ni muhimu sana katika kutekeleza mipango
yetu ya maendeleo na niwaombe wote tuunge mkono jitihada za Serikali.
Nawashukuru sana,
ahsanteni kwa kunisikiliza.
Imetolewa
na:
Idara ya Maendeleo ya
Sekta Binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji,Sehemu ya Uwekezaji,
Ofisi ya Waziri Mkuu
NOVEMBA
15, 2013
No comments:
Post a Comment