TANGAZO


Friday, November 15, 2013

Kombe la Mapinduzi kuanza Januari Mosi hadi 13 mwakani

* Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, azungumza na waandishi wa habari jijini Dar
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) 2014, yatakayoanza Januari Mosi hadi 13, 2014, Visiwani Zanzibar, katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ), Khamis Abdalla Said na katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) 2014, yatakayoanza Januari 1 hadi 13, 2014, Visiwani Zanzibar, katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ), Sharifa Khamis Salim na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo, Visiwani Zanzibar, Nassor Ali Jazira. 
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo, wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akizungumza nao jijini leo.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ), Khamis Abdalla Said, akijibu maswali ya waandishi wa habari, wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk (kulia), alipozungumza nao jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) 2014, yatakayoanza Januari Mosi hadi 13, 2014, Visiwani Zanzibar, katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ), Khamis Abdalla Said, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk (kulia), alipozungumza nao, jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mashindano ya Kombe la Mapinduzi (Mapinduzi Cup) 2014, yatakayoanza Januari Mosi hadi 13, 2014, Visiwani Zanzibar, katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene.
Baadhi ya wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, wakichukua picha na kuandika habari katika mkutano huo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa katika mkutano huo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo, walipokuwa wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Said Ali Mbarouk (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza nao jijini leo, kuhusu mashindano ya Kombe la Mapinduzi yatakayoanza Januari Mosi hadi 13, 2014.

No comments:

Post a Comment