TANGAZO


Friday, November 15, 2013

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Jaji Kiongozi mstaafu, Amiri Manento, aifariji familia ya marehemu Dk. Mvungi

 
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Jaji Kiongozi mstaafu, Amiri Ramadhani Manento, akitia saini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na mpigania haki za binadamu, marehemu Dk. Sengondo Mvungi, Kibamba, Dar es Salaam leo. (Picha zote na Germanus Joseph)
Bibi Fatuma Bakari wa THBUB, akimpa mkono wa pole mke wa marehemu Dk. Mvungi, Bibi Anna Mvungi.
Mhe. Manento akiwa nyumbani kwa marehemu Dk. Sengondo Mvungi huko Kibamba,Kibamba Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji Kiongozi mstaafu, Amiri Ramadhani Manento akimpa mkono wa pole Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. James Mbatia (Mb) nyumbani kwa marehemu Dk. Mvungi, Kibamba Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji Kiongozi mstaafu, Amiri Ramadhani Manento akimpa mkono wa pole Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, Mhe. James Mbatia (Mb), nyumbani kwa marehemu Dk. Mvungi, Kibamba Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Jaji Kiongozi (mstaafu), Amiri Ramadhani Manento akiwa pamoja na baadhi ya viongozi waliofika katika msiba huo jana kwa ajili kuifariji familia ya marehemu Dk. Mvungi. Kulia kwake ni Majaji wa Mahakama ya Rufaa Mhe. Januari Msofe (mwenye miwani) na Mhe. Prof. Ibrahimu Juma.

No comments:

Post a Comment