TANGAZO


Sunday, November 10, 2013

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi (Veta), Phillip Mulugo awa mgeni rasmi mahafali ya VETA Dodoma

Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi, Phillip Mulugo akimkabidhi cheti cha kuhitim mafunzo ya udereva, David Mtutuma aliyemaliza mafunzo katika Chuo cha Veta, mjini Dodoma leo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo, akibishana jambo na wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo cha Veta Dodoma, mara baada ya kumaliza kucheza nao muziki wa Kwaito, wakati wa mahafali hayo, mjini humo leo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip Mulugo akisakata muziki wa Kwaito na wahitimu wa Chuo cha Veta Dodoma leo, ambapo hata hivyo aliibuka mshindi wa kucheza muziki huo kutokana na ustadi mkubwa aliouonesha.
Wahitimu wa kozi mbalimbali wa Chuo cha Veta Dodoma, wakionesha mitindo ya mavazi yaliyobuniwa na mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho kwa wageni na waalikwa mbalimbali waliohudhuria mahafali hayo yaliyofanyika leo, mjini humo.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillip
Mulugo akiwahutubia wahitimu wa Chuo cha Veta, mjini
Dodoma leo.
Mmoja wa wahitimu hao,  Elias Laizel akipongezwa na ndugu zake kwa zawadi na maua  baada ya kuhitimu kozi ya uchoraji na ramani wakati wa mahafali ya chuo hicho cha Veta yaliyofanyika leo mjini Dodoma.
Mhitimu wa kozi ya umeme (Electical instllation),
Gedfrey Manyanga akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo
hayo toka kwa Naibu waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi
Stadi Phillip Mulugo  wakati wa mahafali yaliyofanyika leo
mjini Dodoma.
 Wahitimu wa Veta wakiwa katika mahafali yao hayo.
Baadhi ya wanafunzi wa Veta wakiwa katika mahafali hayo. (Picha zote na John Banda, Dodoma)

No comments:

Post a Comment