Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea msimamo wa nchi yake, wa kuiunga mkono hotuba Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, akisisitiza kwamba Tanzania haitojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pia pamoja na mambo mengine waziri Amina, alisema Serikali yake itashirikiana na Tanzania katika kuiimarisha jumuiya hiyo, kutokana na nchi hiyo na Tanzania kuwa waanzilishi na pia nchi hiyo, kuwa na shughuli mbalimbali za miradi yake nchini. Pia Waziri Amina alisema kuwa nchi hiyo, inaitegemea Tanzania katika sakata la viongozi wake wakuu wa nchi kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo, wakati Waziri mwenzake wa Kenya, Amina Mohamed (kulia), alipokuwa akielezea msimamo wa nchi yake, wa kuiunga mkono hotuba Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, akisisitiza kwamba Tanzania haitojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pia pamoja na mambo mengine waziri Amina, alisema Serikali yake itashirikiana na Tanzania katika kuiimarisha jumuiya hiyo, kutokana na nchi hiyo na Tanzania kuwa waanzilishi na pia nchi hiyo, kuwa na shughuli mbalimbali za miradi yake nchini. Pia Waziri Amina alisema kuwa nchi hiyo, inaitegemea Tanzania katika sakata la viongozi wake wakuu wa nchi kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Baadhi ya viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kushoto) na wa Kenya, Amina Mohamed, wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari, dar es Salaam leo, kuelezea msimamo wa nchi zao katika kushirikiana na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) na pia kuiunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa Bungeni hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe, akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Waziri mwenzake wa Kenya, Amina Mohamed, aliyeelezea msimamo wa nchi yake, wa kuiunga mkono hotuba Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa Bungeni hivi karibuni, akisisitiza kwamba Tanzania haitojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), pia pamoja na mambo mengine waziri Amina, alisema Serikali yake itashirikiana na Tanzania katika kuiimarisha jumuiya hiyo, kutokana na nchi hiyo na Tanzania kuwa waanzilishi na pia nchi hiyo, kuwa na shughuli mbalimbali za miradi yake nchini. Pia Waziri Amina alisema kuwa nchi hiyo, inaitegemea Tanzania katika sakata la viongozi wake wakuu wa nchi kupelekwa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC).
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, akisisitiza jambo katika mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, akitoa ufafanuzi kwa yaliyotokea kati ya nchi yake, Uganda na Rwanda, wakati alipoulizwa na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzani na pia suala la kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, akifafanua kwa waandishi wa habari kwa yaliyotokea kati ya nchi yake, Uganda na Rwanda, wakati alipoulizwa na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi yake na Tanzani na pia suala la kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Viongozi waandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Tanzania wakisikiliza maelezo ya msimamo wa nchi za Tanzania na Kenya yaliyokuwa yakitolewa na Mawaziri wake wa Mambo ya Nje, Bernard Membe na Amina Mohamed.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Amina Mohamed, akisisitiza jambo wakati akizungmza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kazini kwenye mkutano huo na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Kenya, Amina Mohamed, Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kushoto), akimsindikiza mwenzake wa Kenya, Amina Mohamed, mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kushoto), akimsindikiza mwenzake wa Kenya, Amina Mohamed, mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Kenya, Amina Mohamed, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Kenya, Amina Mohamed, wakishikana mkono mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaamleo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Kenya, Amina Mohamed, wakishikana mkono kutakiana heri mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe na wa Kenya, Amina Mohamed, wakiagana mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zao na kuiimarisha Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kutokana na kuwa nchi zao ndio waasisi na waanzilishi wa jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa mkutano huo jijini leo.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Bernard Membe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya yeye na mwenzake wa Kenya, Amina Mohamed kuzungumza na waandishi wa habari jijini leo.
No comments:
Post a Comment