TANGAZO


Saturday, November 9, 2013

Mabondia Said Mbelwa, Shaaban Kaoneka wapima uzito kwa mpambano wao wa kesho Pugu Kilumba

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi ambaye ni mratibu wa pambano kati ya Shabani Kaoneka (kushoto) na Said Mbelwa, Rajabu Mhamila 'Super D' (katikati), akiwainua mikono juu mabondia hao baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao huo, utakaofanyika kesho, Novemba 10, ukumbi wa Zulu Paradies Pugu, Kilumba. (Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Bondia Shabani Kaoneka (kushoto) na Said Mbelwa (kulia), wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito leo kwa ajili ya pambano lao hilo. Katikati ni mratibu wa mpambano huo, Rajabu Mhamila 'Super D'.


Bondia Said Mbelwa, akipima uzito kwa ajili ya pambano lao hilo. Kushoto ni mpinzani wake, Shabani Kaoneka na kulia ni mratibu wa mpambano huo, Rajabu Mhamila Super D'. Mpambano huo, utafanyika kesho Jumapili, Novemba 10, ukumbi wa Zulu Paradies, Pugu Kilumba.

Bondia Shabani Kaoneka, akipima uzito kwa ajili ya mpambano wao huo. Kushoto ni mpinzani wake, Said Mbelwa na kulia ni mratibu wa mpambano huo, Rajabu Mhamila 'Super D'.

No comments:

Post a Comment