Na Martin Ntemo, Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtaka Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, kuhakikisha kuwa Sheria ya Usalama Barabarani inasimamiwa vizuri, ili kuhakikisha kuwa barabara zinazojengwa nchini zinadumu kwa muda uliokusudiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtaka Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli, kuhakikisha kuwa Sheria ya Usalama Barabarani inasimamiwa vizuri, ili kuhakikisha kuwa barabara zinazojengwa nchini zinadumu kwa muda uliokusudiwa.
Akizungumza katika eneo la Buziku, mkoani Geita,
wakati akizindua ujenzi wa barabara ya Bwanga hadi Biharamulo yenye urefu wa
kilometa 67 leo, Rais Kikwete alisema kuwa Wizara ya Ujenzi ni lazima ihakikishe
inasimamia sheria zilizopo na hasa hii ya kutoruhusu magari yenye uzito uliozidi
viwango vilivyoainishwa katika Sheria Namba 30 ya Mwaka 1973.
Akisistiza umuhimu wa kutunza barabara Rais
Kikwete alibainisha kuwa “adui wakuu watatu wanao sababisha barabara kuharibika
mapema ni; magari yanayobeba mizigo zaidi ya uzito uliowekwa kisheria, ujenzi
duni usiozingatia viwango na kuachwa kwa maji kuzagaa barabarani”.
Wakati huo huo, Rais Kikwete alielezea
kufurahishwa kwa kuanza ujenzi wa mradi huo kwani wapo baadhi ya watu waliokuwa
wakieneza taarifa kuwa sehemu hiyo, ya barabara haiwezi kujengwa lakini
sasa wameumbuka.
Awali akitoa maelezo ya mradi huo Mtendaji
Mkuu wa Tanroads Injinia Patrick Mfugale alielezea kuwa mradi mradi wa ujenzi wa
barabara hiyo kwa kiwango cha lami umegharimu Shilingi bilioni 55 fedha zote
zikiwa zimetolewa na Serikali ya Tanzania. “Mradi huu utajengwa kwa muda wa
miezi 27 na hivyo kukamilika mwezi Februari mwaka 2015” alisema Injinia
Mfugale.
Naye Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Magufuli
alimhakikishia Rais Kikwete kuwa wizara yake itahakikisha kuwa inamsimamia
mjenzi wa mradi huo ambaye ni Kampuni ya Sinohydro Ltd. ya kutoka Jamhuri ya
Watu wa China ili aukamilishe kwa muda na viwango vilivyokusudiwa na bila ya
visingizio vya nyongeza ya gharama.
Akimpongeza Rais kwa kutekeleza ahadi yake,
Waziri Magufuli alibainisha kuwa wananchi wa mikoa ya Geita na
Kagera wamefurahishwa sana kuona kuwa hatimaye barabara hiyo muhimu inajengwa
kwani hiyo ndiyo sehemu pekee iliyokuwa imebaki ikiwa haina lami kwa barabara
inayounganisha mikoa hiyo ya ziwa.
Umati wa wananchi wakiwa wamejitokeza kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili eneo la Buziku, mkoani Geita tayari kwa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (aliyeshika mkasi), akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo. Kushoto kwa Rais ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na kulia kwa Rais ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Alhaj Eng. Mussa Iyombe. Wengine katika picha ni baadhi ya Mawaziri, Wabunge na Viongozi wa Mikoa ya Geita na Kagera walioshiriki katika sherehe hizo. Umati wa wananchi wakiwa wamejitokeza kumlaki Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili eneo la Buziku, mkoani Geita tayari kwa uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli, wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti katika eneo la Buziku, mkoani Geita, wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo.
Lori aina ya Scania la Kampuni ya MAPCO Ltd, likiwa na namba za usajili T 895 AFH/T 226 AGB, kama lilivyokutwa eneo la Manyoni, mkoani Singida, likiwa limekatika katikati kutokana na kuelemewa na uzito wa mzigo lililoubeba. (Picha zote na Martin Ntemo, Geita)






No comments:
Post a Comment