![]() |
| Naibu Katibu Mkuu Bara, Julius Mtatiro |
Nikiwa hapa Johannesburg nikihudhuria mafunzo maalum ya usimamizi wa
uchaguzi, nimejulishwa kwamba huko nyumbani Tanzania(bungeni), waziri wa sera,
bunge na uratibu mhe. Lukuvi ameishutumu CUF kuwa ndiyo ilipendekeza tume ya
warioba ivunjwe mara baada ya kukabidhi andiko la katiba kwa bunge la katiba.
Kulingana na umuhimu wangu katika mchakato huu nikikiwakilisha chama changu mara
kadhaa, nimeona nijitokeze kueleza ukweli uliopo katika jambo husika, hivyo
Naomba kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;
1. Awali, maoni ya namna hiyo yalitolewa na chama chetu mbele ya rais
mwaka 2011 ambapo viongozi wa chama chetu wakiongozwa na makamu mwenyekiti taifa
na mie mwenyewe nikiwepo, walikutana na rais Ikulu jijini DSM mwishoni mwa mwaka
2011.
Mantiki ya maoni ya chama chetu wakati huo ilikuwa kwamba, nini
itakuwa kazi ya tume ikishawasilisha andiko lake kwa bunge la katiba ? Serikali
haikuwa na majibu, maoni yetu yakawa kwamba tume imalize muda wake kuliko
kuendelea kulipwa mabilioni ikiwa serikali inajua hakutakuwa na
kazi.
Maoni haya yalikuwa na lengo hasa la kuhakikisha tunapata katiba mpya
lakini pia matumizi ya fedha yasiyo ya msingi tunaachana nayo.
2. Tokea tulitoa maoni ya namna hiyo, hatukuwahi kukosolewa na chama
chochote, taasisi yoyote au vyombo vya habari. Ikumbukwe maoni tuliyoa ikulu
hayakuwa siri, tuliyasema wazi ba tuligawa nakala kwa vyombo vya
habari.
Baadaye mwaka 2012 mwezi wa Septemba, serikali ilipokuwa inahitaji
maoni juu ya sheria ya mabadiliko ya katiba, wanasheria wa chama chetu
walihakiki maoni tuliyoyatoa ikulu mwaka 2011 na bado wakaona maoni ya ukomo wa
tume ya katiba yalikuwa na mashiko. Waraka huu wa maoni uliopelekwa mara ya pili
ulipokamilishwa na hatua zote za chama niliusaini mimi mwezi Septemba
2013.
Na mwezi wa tatu mwaka 2013 serikali ilipoomba maoni(mimi sikuwepo
ofisini wakati huo), mwanasheria wa chama chetu Twaha taslima aliwasiliana na
mwanasheria wetu wa Zanzibar na wakapitia maoni ya Desemba 2011 na yale ya
Septemba 2012 na kufanya mabadiliko kadhaa, suala ukomo wa tume likabakia kuwa
maoni yetu na mhe. Taslima alisaini waraka kwenda serikalini kuhusu jambo
hili.
Wakati tumetoa maoni haya mara zote hatukuwahi kupingwa na mtu hata
yalipoandikwa na vyombo vya habari.
3. Mjadala wa tume ikome au iendelee, tutakubaliana ulianza kwa nguvu
katikati ya mwaka huu 2013 kabla ya bunge lililoenda kupitisha muswada mbovu.
Katikati ya mwaka huu ndipo chama chetu kilijiridhisha kuw mchakato wa katiba
unatekwa na vigogowa CCM na kwamba tume ikivunjwa patakuwa na madhara makubwa
sana.
Mwisho wa Mwezi mei 2013, chama chetu kilitoa taarifa kwa vyombo vya
habari kikiwashutumu watu wanaoiponda tume ya katiba na kutaka iachwe ifanye
kazi zake kwa uhuru, ni wakati huo pia ndipo chama kilieleza waziwazi kuwa tume
ina umuhimu wa kubaki ili kusimamia na kuwa sehemu ya mchakato uliobakia ili
kuondoa kabisa uwezekano wa vigogo wachache kuuhodhi mchakato huu.
4. Baadaye katika bunge la lilipotisha marekebisho miezi michache
iliyopita, vyama vya CUF,CHADEMA na NCCR vilishirikiana na kupinga masuala
kadhaa likiwemo hili la tume kuvunjwa.kama chama chetu kibgetaka ivunjwe hata
sasa kingesema, lakini hivi sasa tumeona umuhimu wa tume kuwepo na tumesema
hivyo na kupigania hivyo, siyo dhambi hata kidogo.
Nani anataka chama chetu kiwe na mawazo yaleyale kila wakati na
kujifunga na ukake katika jambo ambalo tumlipima na kuona madhara yake?
Msimamo wetu wa kutaka tume ibakie umekuwepo tokea mwezi Mei mwaka huu na ni kabla ya ushirikiano wa bungeni na tulipokaa na wabunge wetu kabla ya bunge lile waliekezwa kwenda kupigania tume iendelee kuwepo, na ndiyo maana ilikuwa rahisi kushirikiana na CHADEMA na NCCR kwa sababu tayari pana masuala mengi tulijikuta tuna mtizamo unaofanana.
5. Maneno haya aliyosema Lukuvi jana bungeni alianza kuyasema siku
wakuu wa vyama sita vyenye wabunge walipokuwa Ikulu kuonana na rais. Wakati rais
anafafanua hoja ya uwepo au ukomo wa tume ya katiba ambapo alianza kueleza
umuhimu wa tume kuendelea kuwepo, Lukuvi aliingilia kutaka kumtoa rais kwenye
hoja yake, Lukuvi akajenga hoja kuwa CUF ndo walipendekeza tume ivunjwe. Rais
alimkataza Lukuvi na akamwambia kuwa hayo yalikuwa maoni ya chama na
yalishapita, kwa sasa tuangalie hoja zilizoko mezani na hasa hoja ya vyama vyote
kuwa tume iendelee kuwepo.
Lukuvi aliendelea kujenga hoja kuwa hata kipengele "hatari" cha
kupitisha vipengele vya katiba kwa kutumia wingi mdogo(simple majority)
ulipendekezwa na CHADEMA kupitia kwa Halima Mdee ambaye alipigania utaratibu huo
na kamati ya bunge ikaukubali na kuupitisha.
Lukuvi alipokaa kitako na nyaraka zake mie nikapewa nafasi na
nikaeleza kikao msingi wa maoni yale na nikasisitiza kuwa "yalishapitwa na
wakati" na nikaeleza kwa nini hivi sasa tunataka tume iendelee kuwepo na nikatoa
sababu tunazosimamia.
Mimi na Mnyika tuliongoza mazungumzo ya kamati ya vyama na ile ya
serikali ambapo upande wa serikali waliongozwa na Lukuvi na kuna masuala ambayo
tulikubaliana na kuna yale ambayo hatukukubaliana. Kwa mfano hili la ukomo wa
tume sisi tumepigania tume iendelee lakini kamati ya serikali ikakataa kata
kata, sasa kama wanasema wanataka ivunjwe kwa sababu CUF ilishauri, je mbona CUF
inaposema isivunjwe wao wanakomalia kuivunja? Huu ni uchuro.
5. Watu wanataka kuleta hoja hii iliyopitwa na wakati leo hii. Ikiwa
tunahukumiana kwa maazo tuliyowahi kutoa, mbona serikali kila kukicha inakuja na
mawazo mapya kupinga mawazo ya zamani? Mbona kila mara wanakuja na sheria mpya
kuondoa na kupinga za zamani?
Na kama tunahukumiana, mbona CHADEMA wameoigania mfumo wa serikali za
MAJIMBO tangu wamekuwa chama cha siasa, lakini hivi sasa wameona mfumo huo sio
muhimu na wanasimamia mfumo wa serikali tatu. Je ni nani anayetaka vyama vya
siasa na viongozi wake, wajifunge kwenye ukale na wasifikiri kwa mujibu wa
wakati uliopo?
6. Hoja hii ya Lukuvi inaweza kuwa na lengo la
kuupotosha umma na kuwagawa watanzania na hasa kugawa "spirit" ya vyama vya
upinzani na wananchi kwa ujumla, kuwa CUF ilikuwa na lengo la kuhujumu mchakato
wa katiba, jambo ambalo ni upuuzi usiopaswa kufikiriwa.
CUF imekuwa ni chama pekee kilichopigania mabadiliko ya katiba ya nchi hii kwa kuungana na vyama, taasisi na wafau wote bila kusita, tangu chama kilipoanzishwa, na tutasimama imara kuendeleza mapambano hayo bila kuangalia nyuma.
Suala la hoja fulani kuwahi kupendekezwa namna
fulani na chama fulani wakati fulani na kwamba hivi sasa chama husika
kinashikilia hoja nyingine ni jambo endelevu na si jipya(mawazo ya vyama vyote
duniani) hubadilika kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Kwa sasa mawazo na maoni ya CUF juu ya uwepo
wa tume ya katiba yako wazi sana. TUNATAKA TUME IENDELEE KUWEPO na tumependekeza
juzi katika majadiliano na serikali kuwa WAJUMBE WA TUME WOTE AU BAADHI YAO KWA
KADRI ITAKAVYOONEKANA INAFAA wawe sehemu ya wajumbe wa bunge la
katiba.
Ikiwa LUKUVI ati anatuhukumu kwa maoni ya kale
atakuwa ni waziri na kiongozi wa serikali mwenye maono, busara na uwezo wa
kufikiri mdogo sana. Asitumie mwanya huu ambao uko wazi kujaribu kuichonganisha
CUF na watanzania ambao wanategemea sana mchango wa CUF katika ustawi wa
demokrasia ya kweli na maendeleo ya nchi yetu.


No comments:
Post a Comment