TANGAZO


Saturday, November 16, 2013

Brotherhood yataka majadiliano

 

Wanajeshi wanalinda ikulu wakati wa maandamano awali mwezi Novemba
Ushirikiano wa vyama vya Kiislamu vya Misri ambao haukubali kuondoshwa madarakani kwa Rais Mohamed Morsi umependekeza mazungumzo kujaribu kumaliza msukosuko wa kisiasa nchini humo.
Ushirikiano huo unaoongozwa na Muslim Brotherhood, umetoa taarifa kusihi - kama ilivosema - wanamapinduzi wote, vyama vya kisiasa na wazalendo wajadiliane kwa kina.
Taarifa hiyo haikudai wazi kwamba Bwana Morsi arejeshwe kuwa rais, lakini kwa mara nyengine imelaani hatua iliyochukuliwa na jeshi na kuielezea kuwa mapinduzi.
Brotherhood imekuwa ikidai Bwana Morsi arudishwe madarakani, ingawa vyama vengine katika ushirikiano huo havikudai hayo.

No comments:

Post a Comment