TANGAZO


Saturday, November 16, 2013

Rais wa Sri Lanka hataki uchunguzi

 




Rais Rajapakse na Prince Charles katika ufunguzi wa mkutano wa Jumuia ya Madola, Colombo, Sri Lanka

Rais wa Sri Lanka, Mahinda Rajapakse, ameutoa maanani kwa ukali wito wa waziri mkuu wa Uingereza, David Cameron, kwamba wajumbe wa kimataifa wachunguze madai ya uhalifu uliofanywa mwisho wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo, vilivyomalizika mwaka 2009.
Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuia ya Madola mjini Colombo, Rais Rajapakse alisema wafanye wao, wakifanya wenzao huwa mwao ("wanaoishi kwenye nyumba za vigae hawafai kuwarushia mawe wengine.")
Katoa kauli hiyo baada ya Bwana Cameron, ambaye anahudhuria mkutano huo, kusema kuwa Uingereza itahimiza kufanywe uchunguzi wa kimataifa iwapo Sri Lanka yenyewe haikuanzisha uchunguzi usiopendelea upande wowote.
Alitaja safari ya Bwana Cameron siku ya Alkhamisi katika eneo la Jaffna liloharibika wakati wa vita.
Bwana Rajapakse alisema aliruhusu wageni wake kuzuru eneo la kaskazini kwa sababu Sri Lanka ni nchi huru.

No comments:

Post a Comment