Jitihada za uokoaji zimesitishwa kwa muda baada ya paa la jengo
la maduka lililokuwa linajengwa kuporomoka nchini Afrika Kusini.
Watu wapatao 30 wameokolewa, baadhi yao wakiwa katika hali ya taharuki.
Kepteni Zwane amesema watu 11 miongoni mwa waliopelekwa hospitali wamejeruhiwa vibaya.
Naibu meya wa mji wa Tongaat ameviambia vyombo vya habari vya Afrika Kusini kuwa serikali ilipata amri ya mahakama mwezi mmoja uliopita, kusitisha ujenzi katika eneo la Tongaat, ambao ni mji mdogo uliopo kilomita 40 kaskazini mwa Durban.
No comments:
Post a Comment