Meya wa mji wa Toronto nchini Canada, Rob Ford, ameasi ulevi
baada ya ‘kuokoka’. Jambo hili limetokea baada ya makansela wa baraza la jiji
kumpunguzia madaraka yake.
Bwana Rob Ford mwenye umri wa miaka 22 anasema ameamua kuasi pombe, baada ya
kuokoka na kumtambua Yesu huku akisema kuwa kamwe hatawahi kuonja tone la
pombe.Waziri mkuu wa Canada, Stephen Harper alisema kuwa madai dhidi ya Bwana Ford ni ya kusikitisha sana .
Meya huyo alikabiliwa na shinikizo kujiuzlu baada ya kukiri kuwa aliwahi kutumia dawa ya kulevya aina ya cocaine wakati alipokuwa mlevi chakari.
Pia anakabiliwa na madai ya kumtongoza mfanyakazi wake mmoja wa kike pamoja na kutumia lugha chafu, kuwatisha wafanyakazi wake na kuwa na uhusiano wa kimapanzi na kahaba.
Kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari nchini humo, Ford alisema hajaonja mvinyo kwa wiki tatu na kuwa hatawahi kamwe kunywa pombe.
"Nimeweza kumtambua Yesu kama mwokozi wangu.,’’ alisema Ford.
No comments:
Post a Comment