TANGAZO


Wednesday, November 20, 2013

Iran kuendelea na azma ya Nuklia

 

Rais Barck Obama wa Marekani
 
Kiongozi wa kiroho nchini Iran, ameonya kuwa nchi yake kamwe haitasitisha azma yake ya kuwa na nguvu za nuklia huku ikijiandaa kwa mazungumzo mapya na viongozi wa dunia mjini Geneva.
Ayatollah Ali Khamenei amesema kuwa hatajihusisha moja kwa moja na mazungumzo hayo, lakini amewawekea vikwazo waakilishi wake kwenye mazungumzo hayo.
 
Wakati huo huo, Rais Barack Obama amewataka wabunge wa baraza la Seneti la Marekani kutoiwekea vikwazo zaidi Iran, ili kuyapa muda mataifa makubwa kukamilisha mkataba na Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani ameonya kwamba iwapo mkataba na Iran hautaafikiwa, Iran itaendelea kurutubisha nishati ya urani.
Wajumbe kutoka mataifa sita yataanza awamu mpya ya mazungumzo na Iran mjini, Geneva, Uswisi, siku ya Jumatano.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran amesema anaamini kuwa masuala hayo yatapata ufumbuzi.

Katika taarifa ya video iliyotumwa katika tovuti ya YouTube, Javid Zarif amesema: "Tunatarajia na tunataka heshima yetu. Kwa sisi Wairan, nishati ya nyuklia si suala la kujiunga na kundi fulani au kutishia usalama wa wengine. Nishati ya nyuklia ni kupigia hatua, hatua mbayo itatuwezesha kuamua hatima yetu badala ya kuruhusu wengine kutuamulia."

Rais Obama amekuwa na mazungumzo na maseneta katika Ikulu ya Marekani Jumanne, akiwa pamoja na waziri wa mambo ya nje John Kerry na Mshauri wa Usalama wa Taifa,Susan Rice.

Katika siku za karibuni baadhi ya wajumbe wa baraza la seneti wameelezea wasiwasi wao kuwa Ikulu inakwenda haraka mno kuhusu kuilegezea vikwazo Iran na badala yake wamesema Marekani inabidi ichukue msimamo mkali dhidi ya nchi hiyo.

"Tuna nafasi ya kusitisha mpango wa nyuklia wa Iran na kuurejesha katika masuala ya msingi, wakati ikichunguzwa kama ufumbuzi thabiti utapatikanahusu suala hilo," Ikulu ya Marekani imesema katika taarifa yake.

Taarifa hiyo imesema kama hapakuwa na makubaliano ya awali, Iran itaongeza urutubishaji wa madini ya urani na kufanikisha uzalishaji wa vinu vya plutonium katika mji wa Arak.
Wanafunzi wa Iran waliandamana katika mji wa Qom ili kutetea mpango wa nyuklia.

Waziri wa Habari wa Marekani Jay Carney amesema Bwana Obama aliwaambia maseneta kuwa vikwazo vipya vitakuwa vikali zaidi iwapo Iran itakataa kukubali mkataba mpya unaojadiliwa sasa au waukubali halafu washindwe kuutekeleza.

Rais Obama pia amekanusha taarifa kwamba Iran itapewa dola bilioni 40 (£25bn) ili kuipunguzia vikwazo.

No comments:

Post a Comment