TANGAZO


Sunday, October 6, 2013

Yanga yaipiga 2-0, Mtibwa Sugar Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

Mashabiki wa Yanga wakifuatilia mchezo kati ya timu yao hiyo na Mtibwa Sugar, Uwanaja wa Taifa, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom. Yanga ilishinda mabao 2-0. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Frank Domayo wa Yanga, akimtoka Paul George wa Mtibwa, wakati timu zao zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. Katika mchezo huo, Yanga ilishinda mabao 2-0.
Matokeo ya mchezo huo, yakionekana Yanga mabao 2 na Mtibwa Sugar 0. Matokeo yaliyodumu hadi mwisho mwa mchezo huo.
David Luhende wa Yanga, akipiga mpira huku akizongwa na Paul George wa Mtibwa Sugar katika mchezo huo.
Shaaban Kisiga wa Mtibwa Sugar, akimpiga chenga Didier Kavumbagu wa Yanga.
 Kisiga akimtoka Kavumbagu katika mchezo huo.
Said Bahanuz wa Yanga akipambana na Salim Abdallah wa Mtibwa Sugar.
 Shaaban Nditi, amkitoka Said Bahanuz wa Yanga.
Golikipa Hussein Shariff wa Mtibwa Sugar, akiudaka mpira uliokuwa ukikimbiliwa na Didier Kavumbagu wa Yanga.

Mrisho Ngassa (wa pili kushoto) wa Yanga, akishangilia  na wenzake baada ya kuifungia bao la kwanza timu yake hiyo, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa dhidi ya Mtibwa Sugar, Dar es Salaam leo.

Mrisho Ngassa wa Yanga, akishangilia kwa kunyanyua mguu juu akiwa na wenzake baada ya kutoa pasi kwa Didier Kavumbagu (kulia), iliyozaa bao la pili la timu hiyo katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment