TANGAZO


Sunday, October 6, 2013

Makamu wa Rais Dk. Ghari Bilal afungua Kongamano na Mkutano wa Madaktari wanafunzi jijini Mwanza

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa Nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania (TAMSA), lililofanyika jijini Mwanza leo, Oktoba 6, 2013. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Afya, Dk. Hussein Mwinyi (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Eng. Evarist Ndikilo, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa kabla ya kufunguliwa kwa Kongamano hilo.
 Baadhi ya wanafunzi Madaktari, wakijumuika kuimba wimbo wa Taifa, kabla ya kuanza kwa Kongamano hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea cheti kutoka kwa Mratibu wa Kongamano la Sita la Kimataifa la Madktari Wanafunzi, lililofanyika sambamba na Mkutano wa nne wa Chama cha Madaktari Wanafunzi Tanzania (TAMSA), ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha Hubat Kairuki cha Dar es Salaam, Helga Mutasingwa, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa Makamu wa Rais katika kufanikisha Kongamano hilo. Makamu alipokea cheti hicho, leo Oktoba 6, 2013 baada ya kufungua rasmi kongamano hilo, jijini Mwanza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi Madaktari, baada ya ufunguzi rasmi wa kongamano hilo jijini Mwanza leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mwanza, Anthony Dialo na baadhi ya viongozi wa mkoa huo, baada ya kulifungua kongamano hilo, jijini Mwanza leo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya wanafunzi Madaktari baada ya kulifungua kongamano hilo, jijini Mwanza leo.

No comments:

Post a Comment