Rais Jakaya Kikwete (kulia), akisalimiana na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, wakati walipotembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana yatima, wanaoishi katika mazingira hatarishi ya Wama Nakayama, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani jana. Katikati ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dk. Ramadhani Dau.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akizungumza jambo na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Dk. Ramadhani Dau (katikati), wakati wa ziara hiyo jana.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwalimu wa masomo ya Kiingereza na Uraia wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya watoto yatima, wanaoishi katika mazingira hatarishi (WAMA Nakayama), Sophia Shafii wakati alipotembelea shule hiyo, leo wilayani Rufiji, mkoani Pwani.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (wa tatu kushoto) na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada ( wa pili kulia) wakitia saini mkataba wa msaada wa kutayarisha vifaa vya maabara, ujenzi wa zahanati na kutoa mtambo wa maji wa kutumia jenereta, wenye thamani ya sh. milioni 170 kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana, yatima wanaoishi katika mazingira hatarishi (WAMA Nakayama). Kulia wa kwanza ni Rais Jakaya Kikwete na kushoto wa pili ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Ramadhani Dau. Kushoto, wa kwanza ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Suma Mensah. Hafla hiyo fupi, imefanyika jana, katika shule hiyo, iliyopo wilayani Rufiji, mkoani Pwani.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akionesha mkataba aliosaini pamoja na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okad (wa pili kulia), kusaidia vifaa vya maabara, ujenzi wa Zahanati na mtambo wa maji wa kusukumwa na jenereta, wenye thamani ya jumla ya sh. milioni 170 kwa shule hiyo. Kulia ni mumewe, Rais Jakaya Kikwete, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Suma Mensah (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi ya shule, Dk. Ramadhani Dau.
Rais Jakaya Kiwete (katikati), akitembelea shule hiyo, iliyopo wilayani Rufiji, mkoa wa Pwani. Kushoto anayemtembeza ni Mwalimu Mkuu wa shule, Suma Mensah na kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya shule, Dk. Ramadhani Dau.
Rais Jakaya Kiwete, akisoma moja ya kitabu cha somo la Fizikia katika maktaba ya Shule ya Sekondari ya Wasichana, yatima, wanaoishi katika mazingira hatarishi (WAMA Nakayama) jana, iliyopo wilayani Rufiji mkoa wa Pwani wakati alipotembelea shule hiyo katika ziara yake. Kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Suma Mensah.
Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete (aliyevaa kitenge), akizungumza jambo na Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada (wa pili kushoto), wakati alipokuwa akitembelea Shule ya Sekondari ya Wasichana, ya yatima, wanaoishi katika mazingira hatarishi (WAMA Nakayama). Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo, Ramadhani Dau.
Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (Wama), Daudi Nasib (katikati), akibadilishana mawazo na Naibu wa Waziri wa Chakula (kulia), Adam Malima na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, wakati wa hafla hiyo. (Picha zote na Magreth Kinabo, Maelezo)
No comments:
Post a Comment