NA
MAGRETH KINABO – MAELEZO
Dk Hussein Mwinyi |
WAZIRI wa
Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi amewataka waganga wa tiba asili
washirikiane na wataalamu wa utafiti ili kuwezesha upatikanaji wa dawa bora na
salama.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Waziri huyo wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya siku
ya tiba ya asili ya mwafrika ambayo huadhimishwa kila mwaka Agosti 31, lakini
mwaka huu hayakufanyika kutokana na uhaba wa fedha. Maadhimisho hayo
yanatarajiwa kufanyika mwakani kipindi katika hicho.
“ Tanzania
tunayo mitidawa mingi na mingi haijafanyiwa kazi katika utafit na kuweza kubaini
uwezo wa kutibu magonjwa mbailmbali tatizo lililopo ni jinsi gani mitidawa hiyo
inweza kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama kwa watumiaji kwa kuziwekea
mifumo ya huduma za afya ili kila mwenye kuhitaji aweze kuzipata,” alisema Dk.
Mwinyi .
Dk. Mwinyi aliwataka waganga hao
kushirikiana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu (NIMR) na Taasisi ya
Utafiti wa Dawa za Asili iliyokpo katika Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shiriki- (MUHAS).
Aliongeza
kuwa waganga wote wa tiba asili na tiba ya kisasa wanatakiwa kufanya kazi kwa
kuelewana ili kuwezesha kupata taarifa za awali kabla ya utafiti kamili
kufanyika.
Aliitaja kauli mbiu ya maadhimisho
hayo kuwa ni ‘ Tiba Asili : Utafiti na Maendeleo’ kuwa inalenga kutoa
majukumu kwa waganaga wa tiba asili na tiba mbadala katika sula
zima la utafiti. Pili inatoa changamoto juu ya uendelezaji wa taarifa za utafiti
wa mitidawa katika kutafuta dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali.
Aidha aliwahimiza waganga wa tiba
asili kufanya kazi zao kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao na huduma za
afya.
No comments:
Post a Comment