TANGAZO


Saturday, October 26, 2013

Walinzi kadha wa Iran wauwawa mpakani

 

Msafara wa magari Saravan, Iran
Shirika la habari la taifa la Iran, IRNA, limearifu kuwa walinzi 17 wa mpaka wameuwawa katika mapambano na watu waliokuwa na silaha, kwenye mpaka wa Iran na Pakistan.
 
IRNA imeeleza kuwa baada ya shambulio hilo watu 16 wamenyongwa - watu wenye uhusiano na makundi yenye uhasama na serikali.

Kisa hicho cha mpakani kimetokea kwenye eneo la milima nje ya mji wa Saravan.
Washambuliaji hawajulikani, lakini mjumbe mmoja wa bunge la Saravan, Hedayatollah Mirmoradzehi, aliwaeleza hao kuwa magaidi wanaopinga mapinduzi.

Mpaka wa Iran na Pakistan huwa na machafuko na eneo hilo ni njia inayotumiwa na wafanya magendo ya mihadarati.

No comments:

Post a Comment