Wakili wa Serikali toka
Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA), Patricia Mpuya akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani), kuhusu maboresho ya Sheria ya Usajili wa Vizazi na Vifo,
itakayowezesha kusogeza huduma za upatikanaji vyeti vya kuzaliwa karibu na
maeneo ya wananchi, pia kuongeza idadi ya wananchi waliosajiliwa, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA),
Josephat Kimaro akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu mikakati ya wakala
hao ya kuongeza idadi ya wananchi
waliosajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa nchini, wakati wa mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Afisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO), Georgina Misama. (Picha zote na Eliphace Marwa-MAELEZO)
UTANGULIZI
Cheti cha kuzaliwa ni moja ya nyaraka muhimu sana kwamaisha ya
kila mwananchi kwani humsaidia kupata huduma mbalimbali za msingi. Kisheria hii
ni nyaraka pekee inayotambulisha mtu, tarehe aliyozaliwa na hivyo umri
wake.Pamoja na umuhimu wanyaraka hii, bado ni idadi ndogo ya asilimia 23 yaWatanzania
wamesajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa.
Idadi hii ndogo inatokana na sababu za kihistoria kwani huduma
hii imeanza kutolewa kabla ya uhuru na wakati huo ilitolewa kwa wageni tu.Pia sheria
ya usajili inayotumika si rafiki kiasi cha kuwawezesha wananchi wengi kupata cheti
cha kuzaliwa.
MIKAKATI
Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Taasisi ya serikali
iliyo na jukumu la kusimamia usajili wa Vizazi na vifo,umeendelea kutekeleza mikakati
mbalimbali yenye lengo la kuhakikisha idadi ya wananchi waliona vyeti vya kuzaliwa
inaongezeka kwa kusogeza huduma karibu zaidi na maeneo ya makazi ya wananchi.
Mikakati hiyo ni pamoja na
1) Kuipitia na kuiboresha sheria ya Usajili wa vizazi na Vifo
Wakala umeanza mchakato wakuwezesha kupatikana
kwa sheria mpya itakayochukua nafasi ya Sheria ya Vizazi na Vifo sura na 108 ya
mwaka 1920 ambayo ilifanyiwa marekebisho ya mwisho mwaka 2009 inayotumika kwasasa.
Sheria mpya inakusudia kusogeza huduma
za upatikanaji vyeti vya kuzaliwa karibu na maeneo ya wananchi, matumizi ya teknolojia
katika kutuma na kutunza taarifa za usajili, kufanya mapitio ya ada za vyeti vya
kuzaliwa, kuongeza adhabu kwa wanao thibitika kuwa na vyeti bandia vya kuzaliwa,
nk. Rasimuya kwanza ya Sheria mpya imeshatoka na kupiti wa na wadau.
2) MkakatiwaUsajiliwaWatotowalionaUmriChiniyaMiakaMitano(
U5BRI).
Mkakati huu unatekelezwa kwa awamu na
tayari umeanza kutekelezwa katika Mkoa wa Mbeya kuanzia mwezi Julai 2013 na kuonyesha
mafanikio makubwa.U5BRI unategemea kuendelea kuenezwa katika mikoa yote ya
Tanzania Bara.
Nguzo za mkakati huu ni pamoja na
·
Kusajili
na kutoa vyeti kwa watoto chini ya Miaka Mitano katika Ofisi za Watendaji kata
na vituo vya tiba.
·
Kuondoa
ada ya cheti kwa kundi hilo
·
Kutumia
teknolojia ya mawasiliano katika kutuma na kutunza taarifa
3) KupunguzamudawaupatikanajiwaVyetivyakuzaliwa
Miaka ya Nyuma ilimchukua mwananchi si
chini ya mwezi mmoja kuanzia kuomba mpaka kupata cheti cha kuzaliwa.Kwasasa baadhi
ya mifumo imeboreshwa hivyo mwananchi ataweza kuomba nakupata cheti ndani ya
wiki moja.Maboresho zaidi yanaendelea kufanyika ili kupunguza zaidi idadi ya siku.
4) MkakatiwaUsajilinakutoavyetivyakuzaliwakwaWatotoMashuleni
Mipango inaendelea kuanza usajili kwa
wanafunzi wote wa shule za Msingi mkoani Dar es Salaam. Kwa kuanzia zoezi hili litafanyika
katika Wilaya ya Ilala kwa kushirikiana na Idara ya Elimu ya Wilaya.
5) KampenizaUsajilinakutoaVyetivyaKuzaliwakatikaWilaya
Kampeni hizi zimekuwa zikifanyika kwa
muda mrefu na zinaendelea kufanyika katika wilaya mbalimbali. Kwa mwaka huu,kampeni
zimeshafanyika katika Wilaya 15 za mikoa mbalimbali
6) UsajilinakutoaVyetivyaKuzaliwakatikaTaasisi
Wakala umeanza kutoa huduma ya usajili
katika makundi maalumu ambapo hujaza fomu za maombi nakupatiwa vyeti vya kuzaliwa
katika maeneo waliko baada ya kupitia hatua zote stahili.
Mpaka sasa huduma hii imeshatolewa katika
taasisi 42 za Mkoa wa Dar es Salaam nyingi zikiwaTaasisi za Majeshi ya Ulinzi na
Usalama, taasisi za kidini, Wizara, Makampuni na mashirika mbalimbali.
7) ElimukwaUmma
Wakala unaendelea kutoa elimu kwa
wananchi kuhusu umuhimu wa Usajili, wapi huduma zinapatikana, vigezo husika Nk.
Programu mbalimbali za elimu kwa umma zinaandaliwa ili wananchi wajue faida ya kuwa
na cheti cha kuzaliwa
HITIMISHO
Sheria mpya inategemewa kutamka ulazima
wa kila mwananchi kuwa na cheti cha kuzaliwa na kusisitiza matumizi yake katika
sehemu zote zinazohitaji uthibitisho wa umri. Kila mwananchi aliyezaliwa katika
ardhi ya Tanzania Bara anayo haki yakusajiliwa nakupata cheti kwa mujibu wa Sheria.
Asanteni sana,
Imetolewana:IDARA YA MASOKO NA MAWASILIANO
WAKALA WA USAJILI UFILISI NA UDHAMINI (RITA)
No comments:
Post a Comment