*Chaongeza udahili kwa mwaka wa masomo 2013/2014
Chuo
cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma kimetoa mafunzo kwa Watumishi zaidi ya 4,913
toka 2009 mpaka kufikia Septemba 2013 kwa
Watendaji na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, pia idadi ya
walionufaika na mafunzo haya ni kama ifuatavyo:
a) Wenyeviti wa
Vijiji/Mitaa/Vitongoji 3,733
b) Maafisa Watendaji wa Vijiji/Mitaa 282
c) Maafisa Watendaji wa Kata
388
d) Madiwani 327
e) Wawezesha Mafunzo 52
f) Maafisa Elimu
Sekondari 48
g) Wahudumu wa Ofisi 20
h) Wajumbe wa ALAT 18
i) Wakuu wa Idara 45
Pia Chuo kwa kushirikiana
na Taasisi ya Forum syd ya Mwanza, tangu mwaka 2011 kimeweza kutoa mafunzo ya muda mfupi ya
Uwajibikaji wa Kijamii (Social Accountability) kwa watumishi na viongozi wa
ngazi zote za Serikali za Mitaa pamoja na Asasi za Kiraia, wakiwemo Wenyeviti
na Maafisa Watendaji wa vijiji, Vitongoji, Mitaa na Kata, Waheshimiwa Madiwani,
Wakurugenzi na wakuu wa Idara na Vitengo,
Wakuu wa Magereza, Mabenki, TAKUKURU, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala
wa Wilaya na Maafisa Tarafawa Halmashauri za Wilaya za Ukerewe, Magu na Karagwe
.
Mwaka 2009 Chuo cha Serikali za
Mitaa kiliteuliwa na Serikali kuwa Taasisi Kiongozi ya Mafunzo (Lead Training
Institution) katika kuratibu na kusimamia ubora wa mafunzo yatolewayo kwa
watumishi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Kazi hiyo kwa sasa inafanywa na
Chuo kwa kushirikiana na wafadhili. Kwa sasa wafadhili ambao ni JICA na GIZ. Aidha, Mwaka 2012 Chuo cha
Serikali za Mitaa kiliteuliwa na Serikali kutoa mafunzo elekezi (Induction
Courses) kwa watumishi wote wapya wanaoajiriwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Jukumu hilo ni kwa mujibu wa Waraka namba 5 wa Utumishi wa Umma wa mwaka 2012.
Aidha, Chuo kwa
kushirikiana na OWM TAMISEMI, kiliendesha mafunzo ya Semina elekezi ya Makatibu
Tawala wapya wa Mikoa sita (6) ya Tanzania Bara mwezi Mei 2011 na Makatibu
Tawala wa Mikoa yote tarehe 4/7/2011 hadi tarehe 13/7/2011.
Mafunzo haya yamekuwa
yakifanyika hapa Chuoni na Mengine kwenye Mikoa husika ya Watumishi.
Chuo cha Serikali za Mitaa
ni miongoni mwa Taasisi zilizoko chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa
mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994 (Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka
2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuziwezesha Mamlaka za Serikali za
Mitaa nchini kutoa huduma bora zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha
utawala bora, kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.
Madhumuni mahususi ya Chuo ni kuchangia katika uwezeshaji wa
mchakato mzima wa kupeleka madaraka kwa
wananchi, kujenga na kukuza utawala bora, kukuza uchumi na kuondoa
umaskini katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa hapa nchini.
Chuo hiki kimesajiliwa na
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education)
ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia ubora, viwango na uendeshaji wa Vyuo
vya Elimu ya juu na Ufundi visivyo Vyuo Vikuu hapa nchini.
Majukumu ya Chuo
yamegawanyika katika sehemu kuu tatu:-
i) Kutoa mafunzo ya muda mfupi
na mrefu juu ya taaluma, ujuzi, stadi na mbinu za uendeshaji wa Serikali za
Mitaa kwa Viongozi na Watumishi walio katika ngazi mbalimbali za Serikali za
Mitaa;
ii) Kutoa mafunzo juu ya
mabadiliko yanayohusu Serikali za Mitaa kulingana na Mpango wa Uboreshaji wa
Mfumo wa Serikali za Mitaa na;
iii) Kufanya utafiti na kutoa
ushauri kwa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika na watu
binafsi juu ya masuala yote yanayohusu Serikali za Mitaa.
Chuo katika kutimiza lengo
lake la kuwa ndicho Chuo Kiongozi cha Mafunzo katika Mamlaka za Serikali za
Mitaa, kinaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa zinawafikia watumishi
wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa
kupia mafunzo ya kuwajengea uwezo wao kiutendaji na kitaaluma. Pamoja na
jitihada zinazofanywa na Chuo katika utoaji wa mafunzo ya muda mfupi na yale ya
Muda mrefu, bado kinakabiliwa na changamoto moja kubwa kutoka Mamlaka za
Serikali za Mitaa ni uhaba wa fedha za mafunzo kinachopelekea kutofanyika kwa
mafunzo mengi kwa Watumishi ndani ya
Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao ndio Wadau Muhimu.
UDAHILI
Chuo cha Serikali za Mitaa [The Local Government Training Institute] Hombolo , Dodoma kimedahili Wanafunzi 1603 kwa mwaka wa masomo 2013/2014. Idadi hii inajumuisha Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na kujiunga na Astashahada (Basic Technician Certificate courses) na kidato cha sita wanaojiunga na Stashahada (Ordinaly Diploma Courses) katika fani za Uhasibu na Fedha, Uongozi na Uendeshaji katika Serikali za Mitaa, Maendeleo ya Jamii na Menejimenti ya Rasilimali Watu. Idadi hii ya wanafunzi waliodahiliwa na wale wanaoendelea na masomo inafanya Wanafunzi wote kufikia 2,491 kwa mwaka wa masomo 2013/2014.
Idadi
hii ni sawa na ongezeko la asilimia 96.5%
ukilinganisha na jumla ya
wanafunzi 86 waliodahiliwa katika mwaka wa masomo 2007/2008. Kimsingi Idadi ya
Wanafunzi wanaojiunga na Chuo hiki imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka kuanzia
mwaka wa Masomo 2007/2008, kwa sababu zifuatazo:-
a) Kuongezeka kwa kozi kutoka
kozi nne (4) za awali mpaka kozi nane(8) kwa sasa.
b) Kuongezeka kwa Watumishi
Wanataaluma na Waendeshaji kutoka 38 mwaka 2007/2008 hadi 108 mwaka 2013/2014
c) Kuongezeka kwa miundombinu
mipya ya kujifunzia na kufundishia kama ifuatavyo:-
(i)
Mabweni (8) yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 1,620
jumla;
(ii)
Madarasa (8) yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 400
jumla;
(iii)
Ofisi (8) zenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watumishi
10;
(iv) Maktaba yenye uwezo wa
kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;
(v)
Maabara ya kompyuta yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi
300 kwa pamoja;
(vi) Bwalo la chakula na jiko la
kisasa lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 300 kwa pamoja;
(vii) Nyumba za makazi ya
Watumishi (15), yaani daraja A (5) na daraja B(10);
(viii) Ukumbi wa kutolea mihadhara
namba 3 ambao una uwezo wa kubeba watu 576;
(ix) Kumbi za mihadhara namba
moja na namba mbili zenye uwezo wa kubeba watu 400;
Aidha,
Chuo kimeanza ujenzi wa Kituo cha Afya cha kisasa kitakachogharimu kiasi cha shilingi
bilioni 7.8 Lengo kubwa la ujenzi wa kituo hiki ni kuboresha utoaji wa huduma
za afya kwa Wagonjwa wapatao 3000 wajumuiya ya Chuo ikiwemo wanakijiji
waliozunguka Chuo.
Chuo cha Serikali za Mitaa
ni miongoni mwa Taasisi zilizoko chini ya OWM-TAMISEMI na kilianzishwa kwa
mujibu wa Sheria Na. 26 ya mwaka 1994 (Sura ya 396 toleo lililorejewa mwaka
2002). Lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kuziwezesha Mamlaka za Serikali za
Mitaa nchini kutoa huduma bora zitakazowajengea wananchi uwezo wa kuimarisha
utawala bora, kuondokana na umaskini na kuboresha maisha yao.
Madhumuni mahususi ya Chuo ni kuchangia katika uwezeshaji wa
mchakato mzima wa kupeleka madaraka kwa
wananchi, kujenga na kukuza utawala bora, kukuza uchumi na kuondoa
umaskini katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa hapa nchini.
Chuo hiki kimesajiliwa na
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education)
ambalo ndilo lenye mamlaka ya kusimamia ubora, viwango na uendeshaji wa Vyuo
vya Elimu ya juu na Ufundi visivyo Vyuo Vikuu hapa nchini.
Majukumu ya Chuo yamegawanyika
katika sehemu kuu tatu:-
i)
Kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu juu ya taaluma,
ujuzi, stadi na mbinu za uendeshaji wa Serikali za Mitaa kwa Viongozi na
Watumishi walio katika ngazi mbalimbali za Serikali za Mitaa;
ii)
Kutoa mafunzo juu ya mabadiliko yanayohusu Serikali za
Mitaa kulingana na Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa na;
iii) Kufanya utafiti na kutoa
ushauri kwa Serikali Kuu, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mashirika na watu
binafsi juu ya masuala yote yanayohusu Serikali za Mitaa.
Vilevile kinashirikiana na
Vyuo au Taasisi nyingine katika kujiletea maendeleo ya kitaaluma na pia
maendeleo kwa wananchi. Vyuo na taasisi hizo ni kama vile Chuo cha Mipango na
Maendeleo Vijijini (IRDP - Dodoma), Chuo Kikuu cha Dodoma, Taasisi ya SYD-Forum
(Sweden), Chuo Kikuu Mzumbe, Taasisi ya Maendeleo ya Maafisa wa Serikari za
Mitaa (LOGODI - Local Government Officials Development Institute) ya Korea na
Chuo cha Uongozi cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Dar es Salaam).
Vilevile kinashirikiana na
jamii iliyo karibu katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikumba hususani suala la maji kwa wananchi walio
karibu na Chuo, kuchangia madawati na ujenzi wa shule za msingi, kutoa ufadhili
kwa wanafunzi wasiojiweza kifedha ili kuwawezesha kupata mafunzo yatolewayo
hapa Chuoni na huduma nyingine.
Pamoja
na kutekeleza majukumu tajwa hapo juu, Chuo
kinakabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile ubovu wa barabara ya
Ihumwa – Hombolo yenye urefu wa kilomita 27 ambayo haijajengwa kufikia angalau
kiwango cha changarawe hali ambayo inafanya magari yanayotumia barabara hiyo
kuharibika mara kwa mara hivyo kuongeza gharama za matengezo.
Ombi
letu kubwa katika suala hili ni barabara hiyo kutengenezwa kwa kiwango cha
lami.
Imetolewa na:-
Ofisi ya UhusianoChuo Cha Serikali za Mitaa, Hombolo Dodoma
24.10.2013
No comments:
Post a Comment