Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati walipokuwa wakimpokea kwenye
Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana. Makamu amewasili mkoani Kigoma leo kwa
ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Malagarasi katika Wilaya ya
Uvinza kesho. (Picha zote na OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia burudani ya ngoma za asili kutoka kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma,
wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo mchana, kwa ajili ya
kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagarasi kesho katika Wilaya ya Uvinza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akifurahia burudani ya ngoma za asili na kumpongeza mmoja wa wasanii hao, wakazi
wa Mkoa wa Kigoma, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma leo
mchana, kwa ajili ya kuzindua Kivuko kipya cha Mv Malagarasi kesho katika Wilaya
ya Uvinza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza baada ya kukabidhiwa ripoti ya Mkoa wa Kigoma leo mchana.
No comments:
Post a Comment