Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Elius Mwakalinga (kushoto), akieleza
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu Mpango wa wakala hao, wa
kupunguza Matumizi ya fedha za Serikali katika sekta ya Ujenzi kwa kujenga
Ofisi za Serikali, wakati wa mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) leo, jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Miliki, Erasm Tarimo na kulia ni Ofisa Habari wa Idara ya Habari (MAELEZO), Frank Mvungi. (Picha na Hassan Silayo-MAELEZO)
Ø Wakurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo
Ø Ndugu waandishi wa Habari,
Ø Mabibi na Mabwana.
Kwanza kabisa kwa heshima
na taadhima napenda kutumia fursa hii kuwakaribisha wote katika mkutano huu.
Ndugu
wanahabari,
Leo tumekutana hapa kwa
lengo la kupeana taarifa kuhusu mikakati mbalimbali ya Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA). Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) ulianzishwa chini ya sheria Na. 30 ya mwaka 1997 kutokana na
iliyokuwa idara ya Majengo chini ya Wizara ya Ujenzi. Madhumuni ya kuanzishwa kwa Wakala wa Majengo
ni kuboresha huduma zilizokuwa zikitolewa na iliyokuwa idara ya majengo kwa
kutumia rasilimali kutokana na majengo yenyewe bila kutoka Serikalini/Hazina
hatimaye kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kupunguza gharama za uendeshaji serikalini upande wa sekta ya majengo.
Ndugu
wanahabari,
Wakala
wa Majengo unafanya utafiti kubaini gharama zinazotumika kama kodi ya pango
katika ofisi za serikali ili kuhakikisha Serikali inaokoa fedha kutoka katika Wizara
na Taasisi ambazo zinapanga aidha kwa watu binafsi au mashirika. Katika utafiti
unaoendelea imebainika kuwa, Serikali inatumia fedha nyingi katika kodi ya
pango katika taasis zake.
Ndugu
Wanahabari,
Kama ilivyoelekezwa kupitia
Sheria ya Wakala (Executive Agency Act) namba 30 ya 1997, TBA imekasimiwa
jukumu kubwa la kuhakikisha Serikali na Taasisi zake zinapata ofisi pamoja na
kuhakikisha kuwa watumishi wa umma wanapatiwa makazi yaliyo bora na salama. Katika
kuondoa tatizo la uhaba wa Ofisi kwa serikali, Wakala umeamua kutafuta ufumbuzi
kwa kujenga majengo ya ofisi katika mikoa mbalimbali ambayo yatajulikana kama
“TBA Towers”.
Majengo haya kwa kuanzia, yatajengwa
katika “yard” za Ujenzi zilizopo katika mikoa saba ya Tanzania Bara ambayo ni
Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Mtwara, Arusha na Tanga.
Mkakati huu utaiwezesha
Serikali kupunguza kutumia gharama kubwa katika upangishaji wa ofisi na badala
yake fedha hizo zitumike katika maeneo mengine yenye manufaa kwa jamii na
uhitaji mkubwa kama vile afya, elimu, Jeshi n.k.
Ndugu
Wanahabari,
Kama tulivyoeleza awali,
dhumuni kuu la mradi huu ni kuipatia ofisi za kudumu Serikali na taasisi zake.
Upangishwaji wa kila jengo
utagusa maeneo manne katika utaratibu ufuatao:-
·
Eneo
la kwanza litalenga watu
binafsi ambao watapangishwa kwa kodi ya soko ili kuiongezea TBA kipato na kuuwezesha
Wakala kujenga majengo mengine kwa kipindi kifupi pamoja na ukarabati wa
majengo hayo pale inapobidi,
·
Maeneo
mengine mawili
yatalenga kuzipangisha maeneo ya
ofisi Wizara za Serikali pamoja na
Taasisi zake kwa gharama nafuu na;
·
Sehemu
ya nne ambayo ni ya mwisho itatengwa maalum kwa ajili ya matumizi
ya Wizara ya Ujenzi na taasis zake ambazo awali zilikuwa zikitumia ‘yard’ hizo.
Ndugu
Wanahabari,
Manufaa
ya mradi huu ni kama ifuatavyo:
·
Wizara, Idara na Taasis za Serikali (MDAs)
kupata maeneo/nafasi za ofisi zenye uhakika, zilizo bora na salama kwa gharama
nafuu.
·
Maendelezo ya maeneo yaliyochakaa au
yaliyoachwa kwa muda mrefu na hivyo kupendezesha miji yetu.
·
Kubadilisha sura ya “Ujenzi yard” kwani sasa
zipo katika hali mbaya inayoleta picha mbaya kwa Serikali
·
Kuifanya Serikali na taasisi zake kufanya
kazi bila kusumbuliwa na wenye majengo kama ambavyo wamekuwa wakisumbuliwa
wakiwa wapangaji katika majengo ya mashirika na watu binafsi.
·
Kuiongezea Serikali mali (asset)
isiyohamishika na yenye hadhi.
·
Kuimarisha usalama wa mali na nyaraka za
serikali kwa kuondoa adha ya kuhama hama kila wakati.
·
Kupitia mradi huu Wataalam wa TBA
watajengewa uwezo kitaaluma kwa kutumia vitendea kazi vya kisasa na pia kuboresha masilahi yao kwa upande wa
vipato vyao kwa mfano mishahara, posho mbalimbali n.k
Ndugu
Wanahabari,
Upatikanaji
wa fedha za mradi huu
Kulingana na ufinyu wa
bajeti, TBA inatarajia kutekeleza mradi huu kwa njia ya mkopo kutoka katika
Taasisi mbalimbali za fedha pamoja na kushirikiana na wawekezaji katika sekta
ya miliki (real estate developers).
Hadi sasa, TBA tayari
imeishafanya mazungumzo na baadhi ya taasis za fedha zilizopo ndani ya nchi ili
kuweza kupata fedha ambazo zitasaidia kuendeleza mradi huu.
Aidha, TBA inaendelea na
Mazungumzo na wawekezaji mbalimbali ambao wameonyesha nia ya kutaka
kushirikiana na Wakala katika kuwekeza kwenye baadhi ya ujenzi wa majengo hayo.
Ndugu
Wanahabari,
Teknologia
itakayotumika na faida zake
Majengo haya yanatarajiwa
kujengwa kwa kutumia teknolojia ya ‘Tunnel Form work system’ ambayo
imethibitika kuwa ni ya haraka na nafuu zaidi ukilinganisha na Ujenzi wa
kawaida (conversional method system).
Teknolojia hii, ili iweze
kufanya kazi kwa uhakika inahitaji nidhamu ya hali ya juu katika utekelezaji wa
ujenzi hivyo, TBA kwa kuzingatia hilo imeamua kuzishirikisha taasisi nyingine za
Serikali ambazo ni JWTZ (Suma – JKT) Polisi, Magereza, na TBA Brigedi.
Ndugu
Wanahabari,
TBA ilifikiria umuhimu wa
kushirikisha vikosi hivi vya Serikali kwa sababu zifuatazo:-
·
Kusaidia teknologia hii kubaki nchini kwa kuhakikisha
wataalam kutoka taasisi za Serikali wanaipata na kuifahamu; kwani watu binafsi
ambao hufanya biashara; ni rahisi kuitelekeza teknolojia hiyo iwapo wataona
imeibuka biashara nyingine inayolipa zaidi kuliko teknolojia hii/ujenzi au
wanaweza kuipeleka teknolojia hii katika nchi nyingine bila kujali umuhimu wake kwa taifa letu.
·
Vyombo hivi huweza kufanya kazi mbalimbali
za Serikali hata kama kuna wakati Serikali inakuwa haina fedha za kulipa kwa
wakati.
·
Kuongeza umoja na ushirikiano miongoni
mwa/baina ya taasisi mbalimbali za umma,
·
Taasisi hizi zina rasilimali watu wa kutosha
kufanya kazi zinazotakiwa kutekelezwa.
Ndugu
Wanahabari,
Kwa kuhitimisha TBA inapenda kutoa shukrani kwa
ushirikiano ambao mmekuwa mkiuonyesha hususan katika utoaji wa taarifa kwa
umma.Tunaamini mtaendelea kutumia kalamu zenu katika kuelimisha na hata kuutaarifu
umma wa Watanzania mambo mbalimbali mazuri yanayofanywa na serikali yao.
Asanteni kwa kunisikiliza
No comments:
Post a Comment